-

Mufti Zubeir aziomba taasisi kupeleka huduma vijijini

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir ameziomba taasisi mbalimbali kupeleka huduma za kijamii vijijini ambako watu wanakabiliwa na shida nyingi zaidi.

Sheikh Zubeir alitoa wito huo wakati akiweka jiwe la msingi katika Kituo cha Elimu na Malezi ya Yatima cha Zubeiriya katika kijiji cha Mndolwa Korogwe mkoani Tanga hivi karibuni.

Mufti alisema: “Taasisi nyingi zimerundikana mijini hali ya kuwa watu wa huko vijijini wana shida nyingi sana, hivyo ni muhimu taasisi zikawa pia zinaelekeza nguvu zao huku (vijijini).”

Ujenzi huo unaofadhiliwa na taasisi ya Time to Help kutoka nchini Uholanzi kwa kushirikiana na tawi lake la hapa nchini, unatarajia kukamilika Februari mwakani.

Kituo hicho kinatarajiwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo za elimu, maji na kadhalika na kinatajwa kuwa na uwezo wa kulea yatima wapatao 35 kutoka katika kijiji hicho na maeneo ya jirani. Mufti aliishukuru taasisi hiyo ya Time to Help kwa msaada huo mkubwa na kuziomba taasisi nyingine ziige mfano huo.

Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close