-1. Habari1. TIF News

Mufti Z’bar Aishukuru TIF Kwa Msaada Wa Misahafu

NA MWANDISHI WETU.

Mufti wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi, ameishukuru The Islamic foundation(TIF) kwa msaada wa misahafu na juzu ama. Kwa niaba ya Mufti, shukrani hizo zilitolewa na Fadhili S. Soraga ambaye ni Katibu wa Mufti ambapo alisema wamepokea jumla ya masanduku 82 ya misahafu na juzuu, kama alivyoahidi Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahdi. Katika barua yao kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIF, Sheikh Ibrahim Twaha, ilisema: “Kwa dhati kabisa, tunaomba utufikishie shukrani zetu kwa Mwenyekiti na wanajumuiya wa The Islamic Foundation kutokana na msaada huu mkubwa tulioupokea.” Barua hiyo iliendelea kusema, “Ni msaada uliotufikia katika wakati muafaka ambapo madrasa zetu nyingi hapa Zanzibar zina upungufu mkubwa wa misahafu na majuzu.” Mufti huyo wa Zanzibar alisema kuwa watahakikisha msaada huo unawafikia walengwa haraka iwezekanavyo ili kupunguza tatizo hilo la upungufu. Pia Mufti aliahidi kuendeleza uhusiano na TIF ili kuisaidia jamii juu ya masuala mbali mbali.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close