-

Mahafali ya wahitimu ya Elimu ya awali na Darasa la Saba

MWENYEKITI wa taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi amesema kuwa uongozi wa taasisi hiyo upo kwenye mpango mkakati wa kuboresha miundombinu ya shule ya msingi Imaan pamoja na kuboresha taaluma shuleni hapo kwa upande wa masomo ya mazingira pamoja na masomo ya dini.

Kauli hiyo aliisema wakati wa mahafali ya wahitimu wa elimu ya awali pamoja na wale wa darasa la saba wa shule ya msingi Imaan English medium iliyopo mkoani Morogoro.

Aidha Mwenyekiti Aref ameongeza kuwa kwa sasa mipango iliyopo ni kuhakikisha masomo ya dini yanapewa kipaumbele kama ilivyo masomo mengine ili wanafunzi waweze kufahamu mengi zaidi kuhusu dini yao.

‘’Mipango iliyo kuwepo kwa sasa ni kuhakikisha tunaboresha miundombinu ya majengo ya shule yetu ikiwemo na kumalizia msikiti uliyopo hapa shuleni lakini pia tunataka kuboresha taaluma upande masomo ya dini kwa kuongeza muda wamasomo hayo ili watoto wetu wapate nafasi zaidi ya kufahamu dini yao.

Kwa upande wake mkuu wa idara ya elimu wa the Islamic foundation mwalimu Juma Issa ametoa pongezi kwa taasisi ya the Islamic foundation kutathimi na kuona hipo haja ya kuboresha taaluma shuleni hapo katika upande wa dini ili wanafunzi waweze kufahamu zaidi maarifa ya dini yao kama ilivyo falsafa ya shule hiyo.

‘’Tunaishukuru Idara ya da‘awa ya taasisi ya the Islamic foundation kwa kufanya tathimini na kuona umuhimu wa kuyapa muda zaidi masomo ya dini ili watoto wetu wapate muda zaidi wa kujifunza elimu ya dini ambapo kuanzia mwakani watoto watakuwa wakisoma masomo ya kawaida nyakati za asubuhi na kuanzia adhuuri baada ya swala wataingia masomo ya dini kwa mfumo wa madrasa”

Katika maafali hayo wanafunzi walipata nafasi ya kuonyesha mambo mbalimbali juu ya kile wanachojifunza darasani ambapo mgeni rasmi katika maafali hayo mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic foundation alipata nafasi ya kujionea na kusifu mafunzo yanayo tolewa na walimu kwa vijano hao.

 

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close