-

Mahafali ya Madrasatul Haqq

Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi amewataka wazazi na walezi wa kiislam nchini kujitoa kwa ajili na dini yao ikiwa ni pamoja na kuchangia maendeleo ya uislamu.

Mwenyekiti Aref ametoa kauli hiyo katika hafla ya Mahafali ya madarasa ya Haqq inayopatikana Karume mkoani Morogoro na kuongeza kuwa ni muhimu kwa kila mzazi wa kiislam na waislam kiujumla kuona wivu wa maendeleo katika kuchangia mambo mbalimbali ya kjeri.

Alisema kuwa ikiwa wataweza kujiotoa kwa ajili ya dini yao uislamu utaweza kusonga mbele katika Nyanja mbalimbali.

Aidha  Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi amewataka wazazi wenye wanafunzi katika Madrasa kujitoa ili kuweza kuendeleza madrasa hiyo.

“Ni lazima tuone  wivu wa kuweza kuchangia masuala ya maendeleo ya dini yetu na nilazima kila mzazi atoe fedha kwa ajili yam toto wake kupata elimu ya dini”

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taaasisi ya The Islamic Foundation Sheikh Ibrahim Twaha amesema kuwa wazazi na walezi wa kiislamu wanadhima ya  Kusimamia watoto  wao kwa  kuhakisha wanendeleza kile walichoweza kujifunza katika madrasa iyo kipindi ambacho wanakuwa likizo

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Madrasa hiyo Salim Nassoro Binzoo amewataka wazazi kushirikiana kwa pamoja kwa kulipa ada ili kuweza kuendeleza madrasa hiyo. Nao Baadhi ya wazazi wamesema kuwa wameridhishwa na elimu inayotolewa katika madrasa hiyo ya Haqq iliyo chini ya Taasisi ya The Islamic foundation

Hata hivyo Wanafunzi wa madrasa hiyo wamewataka wazazi kuona umuhimu wa kuwapeleka madrasa ili kuweza kupata elimu yenye manufaa hapa duniani na kesho Akhera

Awali wanafunzi wa  madrasa ya Haq Chini ya Taasisi ya The Islamic Foundation waliweza kuonyesha vipaji vyao  vya masomo mbalimbali wanavyojifunza katika madrasa hiyo

Madarasa ya Haqq inayopatikana Mkoani Morogoro Inamilikiwa na Taasisi ya the Islamic foundation na imekuwa ikifanya vizuri katika kuwazalisha vijana wa kiislamu wenye elimu bora ya dini ya kiislam.

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close