-1. Habari2. Taifa

Madhara ya Uvumi kwa Amani na Usalama wa Taifa

Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe wote, na rehema na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad (saw), watu wake wa nyumbani na swahaba wake wote. Ama baada ya hayo:

Ukweli wa mambo ni kuwa, uvumi na kuwaogofya watu kunazingatiwa ni kati ya silaha hatari zinazoiharibu jamii, bali mawili hayo ni kama shoka inayoiharibu dini kwa nje na ndani, na kuwadhuru walinganiaji na ulinganiaji.

Aidha, uvumi hutia upofu na kuwafanya watu waiache haki na njia sahihi. Mwenyezi Mungu anasema: “ ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata pumbao lao tu. Na nani aliyepotea zaidi kumshinda anayefuata pumbao lake bila ya uongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Qur’an, 28:50].

Na madhara ya uvumi ni makubwa kuliko hata kuuwa, kwa sababu uvumi ni nyenzo kuu inayotumiwa kuleta chokochoko, fitina na uasi miongoni mwa watu. Mwenyezi Mungu anasema: “..kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa.” [Qur’an 2:191].

Sababu ya fitina kuwa mbaya zaidi kuliko kuuwa, ni kwa sababu; mauaji hufanyiwa nafsi inayostahiki heshima na kulindwa, ama fitina huharibu heshima, na uharibifu wake hauishii kwa mtu mmoja bali huiathiri jamii nzima. Na mara nyingi silaha hii ya uvumi hutumiwa na watu waoga na ambao husadikiwa na wajinga na wasiotumia akili zao vema.

Kueneza uvumi ni silaha hatari inayoweza kusambaratisha na kuigawa jamii, na kuwafanya watu wadhaniane vibaya na wakose kuaminiana.

Na jamii inayokimbilia sana mambo ya uvumi ni jamii ya watu wajinga, na kupitia ujinga wao husadiki kila kinachosemwa, na hatimae kujikuta wanakariri taarifa za uongo bila kuzichunguza wala kuhoji.

Ama jamii yenye watu wanaojitambua huwa hawashughulishwi na taarifa za uvumi, na ambazo wanajuwa ni katika mitego ya maadui wa Uislamu. Na kwa mantiki hiyo, uvumi hauwashtui wala kuathiri mambo yao.

Na kwa hivyo basi, ni wajibu kwetu kama Waislamu, kila wakati na hasa katika zama hizi ngumu, tuwe kitu kimoja, tusaidiane katika heri na uchamungu, kila mmoja afanikishe upungufu ulio kwa mwingine, juhudi zifanyike katika kuwaunganisha watu na kuwafanya wawe wamoja.

Uislamu unaharamisha kutoa siri za waislamu na mambo yao ya ndani, hasa mambo yanayoweza kuwasaidia maadui kujua nguvu za waislamu, au udhaifu wao ili kuwadhibiti na hatimae kuathiri amani na utulivu wao.

Sambamba na hilo, Uislamu unakataza kueneza uvumi unaogusa heshima, siri au mambo binafsi ya watu. Mwenyezi Mungu anasema kwenye kitabu chake kitukufu: “Kwa hakika wale wanaopenda uenee uchafu kwa walioamini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.” [Qur’an 24:19]. Na hii ndio hukumu ya akhera kwa mtu anayeeneza uvumi. Qur’an imewaita waeneza fitina.

Na maana ya kueneza fitina kilugha ni: kusababisha sintofahamu kubwa. Maana hii pia hutumika katika kueneza uovu na taarifa mbaya zinazosababisha mkanganyiko baina ya watu. Na kueneza fitina ni haramu kutokana na madhara yake kwa waislamu na jamii kwa ujumla.

Mtu anayeeneza fitina anastahiki kupewa adhabu, kama anavyosema Mwenyezi Mungu: “Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu.” [Qur’an 33:60].

Watu wanaoeneza uvumi ni sumu, na kasi yao ni kama moto na kuni, hubadilika kama kinyonga, na hutema sumu kama nyoka, na wanalenga kuharibu na kubeza.

Wanaoeneza uvumi, ni watu wenye tabia mbaya, nafsi mbovu, fikra chafu, wameparama uso, hawana aibu, wamekosa maadili, wanafiki, wanachurura ubaya na tabia mbaya, uadui umetuwama matumboni mwao, hawapumziki mpaka waharibu ni waudhi na ni wakere. Mtu mfitini, ni mharibifu anayeranda ardhini kufanya uharibifu na kuwafanyia watu ubaya.

Uvumi ni uhalifu dhidi ya usalama wa taifa. Na mueneza uvumi ni mhalifu katika dini na jamii yake, kwani anasababisha machafuko kwenye jamii, na wakati mwingine huwa mbaya zaidi kuliko msafirisha dawa za kulevya. Hawa wote wanalenga kumdhuru mwanadamu, bali anayemlenga mtu kisaikolojia huyo ni hatari zaidi.

Nawe waweza kuhuzunika na kukereka sana unapowaona watu wanapokea uvumi mbaya na kuuona kama ukweli, wakichafua macho na masikio yao kwa uvumi wa uongo.

Uislamu umelishughulikia na kulitibu tatizo la uvumi kama ifuatavyo:

Uislamu unauhesabu uvumi kama tabia mbaya na isiyoendana na sifa ya maadili mema, yaliyoletwa na sharia yake tukufu. Dini yetu inahimiza mshikamano, upendo, kusaidiana, kuhurumiana na kusafiana nia. Na kwa hakika hakuna kingine, isipokuwa uvumi umekuja kuporomoa na kuyaharibu maadili tajwa

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close