-

Kuwa Mkarimu Ndani ya Ramadhani

Ukarimu ni sifa miongoni mwa sifa za Allah Ali- yetuka na ni miongoni mwa sifa za Mtume (rehema na am- ani ya Allah zimshukie). Uka- rimu pia ni miongoni mwa sifa za waumini wa kweli.

Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema katika Hadithul quds kwamba Allah amesema: “Enyi waja wangu, kama wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, katika watu na majini, wangesimama katika uwanja mmoja wakaniomba; nikiwapa kila mmoja kile alichokiomba, kisingepun- gua chochote katika yale niliyokuwa nayo isipokuwa ni kama unavyopun- guza uzi uchovywao katika bahari,” (Muslim).

Pia Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Hakika Allah ni Mkarimu, anapenda ukarimu na tabia nzuri na anachukia tabia mbaya.”

Allah ni Mkarimu wa wakarimu, na hakika ukarimu wake huongezeka ka- tika mwezi wa Ramadhani.

Katika Aya iliyofungamana na Aya za funga, Allah Aliyetuka amesema: “Na waja wangu watakapokuuliza habari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya muombaji anaponiomba. Basi na wa- niitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapatekuongoka,”(Qur’an, 2:186).

Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) alikuwa Mkarimu sana kama ilivyothibiti katika Hadithi ya Ibnu Abbas (Allah amridhie) ambaye

amesema: “Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) alikuwa ni mkar- imu wa watu na ukarimu wake ulikuwa ukizidi sana ndani ya Ramadhani wakati anapokutana na Jibril, na alikuwa akikutana naye kila usiku wa Ramadhani. Kwa hakika Mjumbe wa Allah alikuwa akijitolea katika kheri kuliko uPepo wa heri uvumao mfululi- zo,” (Bukhari).

Hapa Mtume amefananishwa na uPepo wa rehema ambao hutumwa kwa ajili ya kuteremsha mvua za kheri zinazokienea kila kitu.

Anas bin Malik (Allah amridhie) amesema: “Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) alikuwa mzuri wa watu, shujaa wa watu na mkarimu wa watu,” (Bukhari).

Ukarimu wa Mtume ulikusanya aina zote za ukarimu, ikiwemo kuji- tolea mali, elimu na nafsi yake katika kuidhihirisha dini ya Allah na kuwaon- goza waja wake, na pia katika kuwafik- ishia manufaa kwa kila njia, iwe kuwal- isha wenye njaa, kuwanasihi na ku- waelimisha wajinga, na kukidhi haja za watu.

Mtume hakuacha kuwa katika tabia hii nzuri katika maisha yake na ndiyo maana tunasoma kuwa mkewe, Bi. Khadija Binti Khuwailid (Allah amri-

dhie) alimfariji Mtume alipopata hofu ya kutokewa na Jibril katika pango la Hiraa kwa kumwambia: “Hapana, sivyo hivyo. Naapa kwa Allah kuwa hatokufedhehesha kamwe. Hakika wewe utaunga udugu, utamsaidia asi- yejiweza, utamwezesha kuchuma yule asiyekuwa nacho, utamkirimu mgeni na utasaidia katika mambo ya haki,” (Bukhari).

Fadhila ya funga ni maradufu kwa sababu ya ukarimu

Unaweza kupata fadhila za kufunga zaidi ya mara moja kwa kuwasaidia waliofunga, wenye kusimama na wenye kumtaja Allah kwa wingi. Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Atakayemfu- turisha aliyefunga atapata ujira sawa- sawa na ujira wake pasipo kupungua chochote katika ujira wa mfungaji,” (Tirmidhi).

Funga na sadaka (ukarimu) vinape- leka peponi

Kutoka kwa Abu Huraira (Allah amridhie), Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Nani miongoni mwenu ameamka na funga hivi leo?” Abubakr akasema: “Ni mimi.” Mtume akasema: “Nani miongoni mwenu amefuata jeneza leo?” Abubakr

a k a s e m a : “ N i m i m i .” A k a s e m a M t u m e : “Nani miongoni mwenu amemlisha maskini leo?” Abubakar akasema: “Ni mimi.” Akasema: “Ni nani miongoni mwenu amemtembelea mgonjwa hivi leo?” Abubakar akasema: “Mimi.” Mtume akasema: “Hayakusanyiki mambo haya kwa Muumini isipokuwa ataingia peponi,” (Muslim).

Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) alimwambia Mu’adh: “Hivi sikujulishi milango ya kheri? Funga ni kizuizi, sadaka hufuta madhambi kama maji yanavyozima moto.” (Tir- midhi).

Pata dua ya Malaika

Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Hakuna siku ambayo hupambazukiwa waja isipokuwa na Malaika wawili huter- emka, mmoja wao husema, ‘Ewe Mola, mpe badala mwenye kutoa.’ Na mwingine husema, ‘Mpe uharibifu mwenye kuzuia,’ (Bukhari na Muslim).

Hii ni dua inayoombwa kwa yule mwenye kujitolea na yule mwenye ku- fanya ubahili. Ni vizuri kujitolea ndani ya mwezi huu ili kuipata dua njema ya Malaika.

Jikinge na moto

Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Hakuna yoyote miongoni mwenu isipokuwa Mola wake atamsemesha pakiwa hakuna mkalimani kati yake na yeye, atataza- ma kuliani mwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza na atatazama kushotoni mwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza. Atakayeweza kati yenu kujikinga na moto angalau kwa nusu ya tende basi na afanye hivyo,” (Bukhari).

Hii ina maana ajitolee hata kama kwa sadaka ya kitu kidogo.

Kuwa mkarimu ili upate zaidi

Imepokewa Hadithi kutoka kwa AbuHuraira(Allahamridhie)kwamba Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amesema: “Allah Ali- yetukukaamesema, ‘Toaewemwan- adamu nami nitakupa,’” (Bukhari).

Allah Aliyetukuka anasema: “Sema, ‘Kwa hakika Mola wangu Mlezi hum- kunjulia riziki na humdhikisha am- takayekatikawajawake. Nachochote mtakachokitoaYeyeatakilipa. Nayeni Mbora wa wanaoruzuku,’” (Qur’an, 34:39)

Kuwa na mkono wa juu

“Mkono wa juu (mwenye kutoa) ni bora kuliko mkono wa chini (mwenye kuomba,” (Bukhari na Muslim).

Ukarimu ni moja wapo ya njia ya kupata mapenzi ya Allah, kwa kuwa ni aina ya ihsan (wema). Na Allah Ali- yetuka anawapenda wenye kufanya ih- san.Allahanatuhimi-

za kusaidiana katika wema na uchaji. Ni wazi kuwa huu ndiyo muda wa kuweze- shana kusaidiana na kuhurumiana, tutoe kwa ajili ya manufaa yetu, dini pamoja na jamii kiujumla.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close