-

Kipyenga cha Misk ya Roho 2018 Kimeshapulizwa…

Mada kuu: ‘Utukufu Wake…’

Katika muendelezo wa mfululizo wa makongamano mbalimbali yanayoandaliwa na taasisi ya The Islamic Foundation (TIF), kwa mara ya pili mtawalia tunawaletea kongamano kubwa kuwahi kutokea katika ukanda wa Afrika Mashariki litakaloendeshwa kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

Misk ya Roho ni kongamano la kidaawah la Afrika Mashariki ambapo TIF, huwaalika masheikh kutoka katika nchi za Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Kongamano la pili la Afrika Mashariki lijulikanalo kama Misk ya Roho 2018 au Misk ya Roho 1440H ambalo limebeba anuani ya maudhui ijulikanayo kama “Utukufu Wake…” litafanyika Oktoba 28, 2018 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Katika kongamano hili tunategemea in shaa Allah watu watakaohudhuria kunufaika kwa mada mbalimbali zitakazowasilishwa na masheikh ambazo kwa kiasi kikubwa zitazungumzia utukufu wa Mfalme wa wafalme, Allah Aliyetukuka kwenye jinsi ya kumpwekesha, majina na sifa zake na jinsi ya kuyatumia katika maisha yetu ya kila siku ili tupate kufaulu.

Masheikh walioalikwa kuhudhurisha mada siku hiyo ni Sheikh Dourmohamed Issa kutoka Tanzania, Sheikh Ally Jumanne kutoka Tanzania, Sheikh Abdulrahman Mhina (Baba Kiruwasha) kutoka Tanzania, Sheikh Yusuf Abdi kutoka Kenya, Sheikh Jamaldin Osman kutoka Kenya, Sheikh Zuberi Bizimana kutoka Burundi, Sheikh Ally Kajura kutoka Rwanda na Sheikh Muhammad Abduweli kutoka Uganda.

Ni orodha ya masheikh wanane wanaojulikana kwa weledi wao katika maswala ya kielimu na uhudhurishaji mada katika hadhara mbalimbali ikiwemo vituo vya televisheni na redio wote utawapata katika mimbari moja wakizungumzia ‘Utukufu wake…’

Kongamano hili linatarajiwa kuanza majira ya saa mbili asubuhi na kumalizika saa 11 jioni, hivyo huduma za kiibada kama Swala zitapatikana hapohapo ukumbini katika eneo maalumu lililotengwa.

Pia, huduma ya chakula na vinywaji itatolewa kwa watu wote watakaohudhuria. Huu ni wakati mzuri wa kupanua mawanda ya mtandao wako kwa kukutana na watu wapya wa kada tofauti kwa siku nzima huku mkifukizwa Misk katika roho zenu.

Katika kuhakikisha taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) inawashirikisha watu katika kupata malipo ya kheri za kuandaa makongamano haya yenye tija kwa jamii yetu, tumeweka utaratibu wa watu kuchangia gharama za maandalizi ya kongamano hili kwa kununua tiketi kwa gharama ya Shilingi elfu tano tu (5,000/=) au kudhamini kwa namna yoyote ile iwezekanayo.

Tiketi za kongamano hili zinapatikana katika vituo vifuatavyo;

 • Kanzu Point na Anezylitta Design-City Mall,
 • GGS Bolts & Nuts-Livingstone Kariakoo,
 • Ibn Hazm Book Store-Kinondoni Mtambani,
 • Car Centre Morocco-Kawawa Road,
 • Yakub Jewellers-Mikocheni Shoppers Plaza,
 • Taste Me-Dar Free Market,
 • Street Soul-Mlimani City, Magomeni Kichangani-Piga simu 0714541 957,
 • Mbagala Rangi tatu Sokoni-Piga simu 0715 328 512,
 • Gongo la Mboto-Masjid Al-Jumaa,
 • Buguruni kwa Mnyamani-Piga simu 0655 611248,
 • Tandika Chihota-Masjid Al-Irshaad.

Pia unaweza kununua kupitia mitandao ya simu ya Tigo Pesa kwa namba 0718 000 433 na M-Pesa kwa 0742 877 775. Unachotakiwa kufanya ni kutuma pesa kiasi cha shilingi 5,000/= kwenda kwa moja ya hizo namba mbili (aidha ya tigo au ya voda) kisha tuma namba yako ya simu na majina yako kamili kwenda kwa namba hiyohiyo. Ukifanya hivyo, utapokea ujumbe mfupi wenye namba yako ya tiketi.Tunza ujumbe huo mpaka siku ya kongamano. Hakikisha jina ni Tajmohamed Shaaban.

Kama una mushkeli, swali au unahitaji maelezo zaidi kuhusu kongamano hili basi tembelea tovuti yetu kwa anuani ya www.islamicftz.org/miskyaroho.  Pia unaweza kutembelea mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter: Islamicftz au wasiliana nasi kwa namba 0653 949 306 (Wanaume tu) au 0625 628 542 (Wanawake tu).

Ni jambo la kushangaza kama wakazi wa Afrika ya Mashariki na Watanzania hususan wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam na viunga vyake watashindwa kutumia fursa hii ya dhahabu ya kuhudhuria katika kongamano hili kwani kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukipata maombi kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na nchi za jirani wakitaka kongamano hili likafanyike huko.

 

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close