-

KARIBU WAHAJ TARIN

Aref Nahdi ahimiza Waislamu wajitokeze kwa wingi

Hatimaye yule Mhadhiri wa Kimataifa kutokanchi ni Australia, ali-yekuwa akisubiriwa kwa hamu, Ustadh Wahaj Tarin anawasili hapa nchini Jumamosi ya wiki hii, InshaAllah; na anategemewa kuendesha mihadhara mitatu mikubwa Dar es Salaam, Morogoro na Visiwani Zanzibar.

Taasisi ya TIF ambayo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Aref Nahdi ndiyo waandaaji wa ziara hiyo inayofadhiliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ). Makampuni mengine yaliyofadhili ziara ya Ustadh Tarin ni pamoja na Benki ya Amana, Kampuni za Bakhresa, Kampuni ya Camel, Lake Oil, Afroil, Morobest, Simbaoil, Tanga Fresh, ATN, O-Gas na Maji ya Afya.

Ratiba ya ziara

Ustadh Tarin anategemewa kuwasili jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi, Aprili 15 na kupokewa na timu nzima ya wenyeji wake kutoka taasisi ya TIF, lakini mhadhara wa kwanza utafanyika kesho yake, siku ya Jumapili.

Ustadh Tarin ambaye licha ya kuwa Mhadhiri wa Kimataifa, pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu nchini Australia, atafanya mihadhara mitatu mikubwa, ukianziwa na ule wa Diamond Jubilee wa Aprili 16 utakaoanza saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana.

Mhadhara wa pili utafanyika Aprili17 mkoani Morogoro katika ukumbi wa studio za Imaan, kuanzia saa mbili na nusu usiku hadi saa tatu na nusu usiku na kumalizia mhadhara wa mwisho Visiwani Zanzibar, Aprili 20, katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sumait kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana.

Sifa za Ustadh Tarin

Ustadh Tarin ambaye anasifika kwa ufasaha wa kuzungumza na ufahamu mpana wa Uislamu, ana Shahada ya Kwanza katika masuala ya Uhandisi wa Uchimbaji wa Metali na Shahada ya pili ya Utawala katika Biashara.

Ustadh Tarin anasifika ulimwenguni kote kwa uwezo wake mkubwa wa kufikisha da’awah na video zake zimeenea katika mitandao mbalimbali mingi ya kijamii, hususan Youtube, zikionesha anavyofikisha ujumbe wa Allah katika nchi mbalimbali duniani.

Ni kutokana na sifa kubwa za Ustadh Tarin na umuhimu wa da’awah ata-
kayoitoa ndiyo maana Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahdi amewataka Waislamu wajitokeze kwa wingi katika mihadhara yote mitatu na kusisitiza kuwa HAKUNA KIINGILIO. “Mwanzo tulitangaza kuwa watu wajisajili mapema lakini tunasema kutokana na umuhimu wa tukio hili watu waje hata siku hiyohiyo ya tukio wasikilize ujumbe wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kupitia mgeni wetu huyu,” Nahdi alisema na kuongeza: “Dar es Salaam jitokezeni, Morogoro jitokezeni na Zanzibar jitokezeni kwa wingi iwezekanavyo.”

Habari nyingine nzuri kutoka TIF zinasema huenda mihadhara hii itaoneshwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni kwa hiyo Watanzania walio mikoa mingine wanaweza kufuatilia katika vyombo hivyo.

Masheikh wazungumzia ujio wake Akizungumzia ujio wa Ustadh Tarin, Katibu Mkuu wa TIF, Sheikh Muhammad Issa amesema ziara yake ita-
wasaidia Waislamu nchini kupata nasaha na mambo juu ya mbalimbali yanayoukabili Uislamu kwa sasa.

“Waislamu tutanufaika na nasaha za Ustadh Tarin na tutaweza kujua changamoto zinazoukabili Uislamu duniani kwa sasa, kwani Tarin ni miongoni wa wahadhiri wenye uwezo wa kuzungumzia hali ya Waislamu kwa kina na mapana yake,” alisema Sheikh Muhammad Issa.

Nao baadhi ya Waislamu waliozungumza na gazeti hili, wamesifu ujio wa Tarin na kusema kuwa wanategemea mambo mengi kutoka kwake huku wakiipongeza TIF kwa kuwaleta wahadhiri wa kimataifa hapa nchini.

“Tunafurahi kusikia Ustadh Tarin anakuja, kwani tunategemea kujifunza mengi kutoka kwake, hususani hali ya Uislamu kwa sasa. Pia hii ni fursa hata kwa wahadhiri wetu nchini kuja kujifunza namna bora ya kufikisha ujumbe wa Allah,” alisema Hussein Muhaji wa Dar es Salaam. Naye Juma Sadiqi alisema TIF inafanya mambo ambayo taasisi nyingi zimeshindwa kufanya. “Kwa kweli TIF imetusaidia sana kuinua upeo wetu wa ufahamu wa Uislamu kwa kutuletea wahadhiri hawa wa kimataifa. Ni faida kubwa kwa Waislamu”.

TIF yatekeleza ahadi

Katibu Mkuu wa TIF, Sheikh Mohammed Issa amesema kuwa ujio wa Tarin unatokana na ahadi ya Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Aref Nahdi wa kumleta mgeni mashuhuri wa kimataifa kila mwaka ili kuzungumza na Waislamu wa Tanzania. Sheikh Muhammad Issa aliwataka Waislamu wahudhurie kwa wingi katika maeneo ambayo mihadhara hiyo itafanyika ili waweze kupata faida katika yale ambayo Ustadh Tarin atayazugumza.

Hii si mara ya kwanza kwa TIF kuleta wanazuoni wakubwa duniani kwa ajili ya kuwalingania Waislamu. Mwaka jana TIF ilimleta nchini muhadhiri wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe, Mufti Ismaili Menk ambaye alifanya mihadhara hapa nchini iliyohudhuriwa na mamia ya Waislamu.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close