-1. Habari1. TIF News

Kamati ya ujenzi masjid Falaah, Kilombero yaishukuru TIF

KAMATI ya Ujenzi wa Msikiti wa Falaah Kilombero KII, mkoani Morogoro imeishukuru Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) kwa ku- saidia ujenzi wa msikiti huo uliozin- duliwa hivi karibu.

Akikabidhi barua ya shukrani kwa Mwenyekiti wa TIF Aref Nahdi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Abubakar Daiy alisema wanashukuru kwa ujenzi wa msikiti, nyumba ya Imam na kitega uchumi cha maduka. Daiy amesema kamati yake inajali mchango mkubwa wa TiF katika ujenzi huo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Nahdi aliipongeza kamati hiyo kwa kuonyesha kujali ujenzi huo na kuwa- taka kuweka mipango mbalimbali ya kuendeleza msikiti huo.

Nahdi alisema, ni vyema msikiti huo

ukawa kituo bora cha dini ya Kiislamu, na kushauri katika kuuendeleza lijeng- we eneo la kuandaa maiti ili kusaidia jamii ya Kiislamu. Nao wajumbe wen- gine wa kamati hiyo waliishukuru TIF kwa kujitoa kusaidia jamii na kuielezea taasisi hiyo kama mfano wa kuigwa. Pia waliwataka Waislamu kujenga utama-

duni wa kuthamini vya kwao ikiwemo kutumia Zahanati ya Saraten iliyopo Mikumi inayomilikiwa na TIF

Msikiti wa Al- Falaah Kilombero KII ulizinduliwa hivi karibuni na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini, Mhesh- imiwa Ibrahim Al Suwaid ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close