-

Jeshi la Polisi Laipongeza Imaan Media

JESHI la polisi mkoani Mor o g o r o l i m e m p o n g e z a Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF), Aref Nahdi kwa jitihada anazozifanya kupitia vyombo vya habari vya radio, televisheni pamoja na gazeti imaan za kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kupambana na uhalifu nchini hususan mkoani Morogoro. Pongezi hizo zimetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro, Ulrick Matei, katika barua yake ya shukran kwa Taasisi ya The Islamic Foundation kwa ushirikiano inayoonyesha kwa Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro ya kukemea vitendo vya uharifu pamoja na kuripoti kwa weledi matukio mbalimbali wanayoyapata kutoka kwa jeshi hilo. Barua hiyo imesema kuwa TIF imekuwa ikifanya kazi kubwa katika kukemea maovu katika jamii na kwamba jeshi hilo linaiunga mkono katika hilo. Akipokea barua hiyo kwa kutoka Jeshi la Polisi kwa niaba ya Mwenyekiti Nahdi, NaibuKatibu Mkuu wa TIF, Sheikh Mohammed Issa amesema TIF itaendeleza ushirikiano na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha vita dhidi uhalifu wote ikiwemo dawa za kulevya inafanikiwa. H i v i k a r i b u n i , Mwenyekiti wa TIF akiwa ziara huko mkoani Kilimanjaro alisema taasisi yake inaunga mkono jitihada za serikali za kupambana na dawa za kulevya na kusisitiza kuwa TIF kupitia vyombo vyake vya habari itendelea kukemea maovu

Tags
Show More

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button
Close
Close