-

JAI watoa msaada wa vyakula Muhimbili na Temeke

Vituo vya Jumuiya ya Wahuishaji Tabia za Kiislamu nchini (JAI) vya Muhimbili na Temeke vimetoa msaada wa vyakula kwa wagonjwa wasio na uwezo waliolazwa hospitalini.

Katibu wa JAI katika kituo cha Muhimbili, Ramadhani Kombo, ameeleza kuwa baadhi ya wagonjwa hawana ndugu na wengine hawana uwezo wa kupata vyakula ndio maana wameamua kutoa msaada huo.

Naye Amir wa JAI kituo cha Temeke, Ally Mbweze amesema msaada huo ni sehemu ya malengo ya JAI na kwamba wataendelea kufanya hivyo. Mbweze pia ametaja shughuli nyingine za JAI kuwa ni pamoja na kugharamia matibabu, kuchangia damu na kuzika maiti wasiyokuwa na
ndugu.

Nao wagonjwa waliopatiwa msaada huo wametoa shukrani zao za dhati kwa JAI na kuwaomba waendelee kujitolea kwa wasio na uwezo.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close