-1. Habari1. TIF News

Hafla ya chakula, TIF na Dar Al Ber society.

Taasisi ya Dar Al Ber Society kwa kushirikiana na TIF, wameandaa hafla fupi ya chakula kwa ajili ya mayatima, kwenye makao makuu ya The Islamic Foundation.

Katika hafla hiyo, wageni kutoka Taasisi ya Dar Al Ber kutoka Dubai wamepata fursa ya kuongea na watoto hao pamoja na walezi wao.

Baada ya chakula, zawadi zilitolewa kwa watoto hao na hafla hiyo kumalizika kwa kutembelea ofisi za Redio na Tv Imaan zilizopo Makao makuu ya TIF mjini Morogoro.

Show More

Related Articles

Back to top button
Close