-

Dkt. Ahmada El Badaoui amesifu juhudi za TIF

#BALOZI wa Comoro nchini #Tanzania Dkt. Ahmada El Badaoui amesifu juhudi za Taasisi ya The Islamic Foundation chini ya mwenyekiti wake Aref Nahdi kwa jitihada kubwa za kuwainua waislamu nchini Tanzania kupitia nyaja mbalimbali ikiwemo kiuchumi,kielimu pamoja na kijamii.

BALOZI huyo aliyasema hayo katika ziara aliyoifanya leo makao makuu ya Taasisi ya The Islamic Foundation na kujionea kazi mbali mbali zinazofanywa na #TIF

Balozi huyo ameisifu #TIF kwa kufanya shughuli zake kisasa na kwa mujibu wa #uislamu unavyotaka na kuongeza kuwa vyombo vyake vya #Habari vimekuwa vikikomboa umma mkubwa wa watu kutokana na #Elimu inayotolewa.

Hata hivyo ameuzungumzia ushirikiano wa nchi ya #Comoro na #Tanzania na kusema kuwa ni mzuri na kwamba unaimarika siku hadi siku na kuongeza kuwa #ushirikiano huo umesababisha kila mwezi kuingia nchini raia wa Comoro wapatao #500 na kwamba ushirikiano wa Tanzania na Comoro umelenga nyaja zote katika ikiwemo kiuchumi,kisiasa pamoja na kijamii
#TvImaan #RadioImaan #Islamicftz

Tags
Show More

Related Articles

Back to top button
Close
Close