1. Habari

Unaufahamu ugonjwa wa seli mundu?

Seli mundu au ‘sickle cell’ ni moja kati ya magonjwa makuu yanayoathiri damu moja kwa moja. Kama jina linavyojieleza, ugonjwa huu ni matokeo ya seli nyekundu za damu kubadili maumbile yake na kuwa kama mundu.Kwa takwimu zilizopo ugonjwa huu huathiri takriban watu milioni nne na nusu duniani kote ambapo asilimia 80 ya wagonjwa hupatikana katika nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara.

Undani wa seli nyekundu za damu

Ugonjwa wa seli mundu huathiri seli nyekundu za damu pekee. Kwa kawaida seli hizi huwa na maumbile ya duara mithili ya lenzi mbonyeo. Maumbile haya ni muhimu sana kwani huziwezesha seli hizi kuwa na uwezo wa kupenya katika mishipa midogo ya damu bila kukwama. Pia maumbile haya yanazifanya seli hizi kuwa na vyumba vya kutosha kwa ajili ya kuhifadhi na kusafirisha hewa ya oksijeni kutoka kwenye mapafu kwenda sehemu nyingine za mwili.

Kwa wagonjwa wa seli mundu, seli hizi hujikunja na kuwa mithili ya mundu au mwezi mwandamo, endapo kiwango cha hewa ya oksijeni kitapungua. Kwa kawaida seli hizi huvunjwa vunjwa na
mwili na pia hunasa kwenye mishipa midogo ya damu na hatimae kusababisha dalili mbalimbali kwa mgonjwa.

Uhusiano wa vinasaba na seli mundu

Ugonjwa huu si wa kuambukiza bali hupatikana kwa kurithi kutoka kwa wazazi wote wawili. Kabla ya kuendelea ni vyema tukaelewa vitu viwili ni tofauti, kuna kuwa na ugonjwa huu (sickle cell disease) na kuwa mbebaji wa ugonjwa huu (sickle cell carrier).

Kuwa na ugonjwa inatokana na kurithi vinasaba vya ugonjwa huu kutoka kwa wazazi wote, ila kuwa mbebaji wa ugonjwa huu ni kurithi vinasaba kutoka kwa mzazimmoja tu. Pia msomaji, elewa ya kuwa mbebaji wa ugonjwa huu huwa hapati dalili yoyote na huishi kama mtu wa kawaida.

Ili mtu apate dalili za ugonjwa huu ni lazima arithi vinasaba vya ugonjwa huu kutoka kwa baba na mama. Vinasaba hivi hurithiwa endapo wazazi wote watakua na ugonjwa huu, au mzazi mmoja ni mbebaji na mwengine ni mgonjwa. Pia, wazazi wote wawili wakiwa wabebaji wanaweza kuchangia nusu nusu ya vinasaba na kuwarithisha watoto watakaowazaa.

Ramani ya Afrika ikionyesha wingi wa uwepo wa watu wabebao vinasaba vya seli mundu

Dalili zake

Watu ambao ni wabebaji wa seli mundu huwa hawapati dalili yoyote kwa sababu
wanakua hawana huu ugonjwa lakini kwa wagonjwa wenye seli mundu huweza kupata dalili mbalimbali ambazo mara nyingi huanza utotoni. Dalili hizi zinaweza kuwa homa za mara kwa mara, mwili kuwa na rangi ya njano; kuvimba mwili hasa miguu, mikono na tumbo kwa watoto; maumivu makali ya mwili hasa tumbo, mgongo pamoja na maungio; kupata ganzi; na pia wengi hupata matatizo ya mara kwa mara ya kupungukiwa na damu.

Mbali na dalili hizi, ugonjwa huu huweza kusababisha dharura ambazo huwa
na matokeo mabaya ikiwa hazitashughulikiwa haraka. Dharura hizi ni pamoja na maumivu makali ya kifua na kushindwa kupumua, tumbo kuvimba na kupungua kwa damu pamoja na kupata
kiharusi.

Tags
Show More

Related Articles

Close
Close