Tag Archives: wema waliotangulia

Tujifunzayo katika maisha ya Salmaan bin Alfaarisy MAISHA YA MASWAHABA: 4

Tunapoipitia sira ya kila Swahaba katika Maswahaba wa Mtume, tunakuta maajabu na mazingatio makubwa yanayogusa maisha yetu kiimani, kifamilia, kiutamaduni na kijamii. Hata hivyo, safari ya Maswahaba ya kuitafuta neema ya Uislamu hutofautiana sana. kwa mfano, safari ya kuufikia Uislamu ya Maswahaba kama vile Abubakr, Uthman, Ali, Abdurahman bin Auf zilikuwa fupi sana, lakini safari ya Swahaba Salmaan [Allah amri- ...

Read More »

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy, Maisha yake baada ya kusilimu

Kutokana na maelezo yaliyotangulia tunajifunza kwamba Salmaan alisilimu mwaka wa kwanza Hijriya mara tu baada ya Mtume [rehema za Allah na amani zimshukie] kuwasili Madina. Kuanzia hapo aliishi na Mtume na inasemekana alikuwa muachwa huru wake, kwa maana Mtume alimlipia gharama za kumkomboa. Na pia Salmaan anatajwa kuwa ni katika watu aliyowapa hadhi yakuwa mtu wa nyumbani mwake [Ahlu bayti]. ...

Read More »

Usia wa Mtume (saw) kwa vijana

Kutoka kwa Alqama amehadithia kuwa, alikuwa anatembea na Abdullah bin Masoud [Allah amridhie] ndipo walipokutana na Uthman bin Affaan [Allah amridhie]. Hapo walisimama wakazungumza naye. [Uthman] Akasema: “Ewe Abuu AbdirRahman kwanini tusikuozeshe kijakazi huenda akawa anakukumbusha baadhi ya yale yaliyokupita.” Abuu AbdirRahman [bin Masoud] akasema: “Ama ikiwa utasema hivyo, kwa hakika Mjumbe wa Allah [rehema za Allah na amani zimshukie] ...

Read More »

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy (as) -2

Kutoka katika kitabu,‘Suwarun min hayati swahaba,’ Salmaan Alfarsiy, Swahaba mtukufu, anaendelea kusimulia, kuwa baada ya kuishi Ammuuriya na mwalimu wake muda aliojaaliwa, ulifika muda wa mwalimu kuiaga dunia. Salmaan Alfaarisy (Allah amridhie) alimuuliza: “Unaniusia nini baada ya wewe kuondoka?” Mwalimu wake akamjibu: “Sidhani kama kumebaki mtu yoyote juu ya mgongo huu wa ardhi aliyeshika dini sahihi hii tuliyoishika sisi. Lakini ...

Read More »

Wala msife ila mmekuwa Waislamu (Qur’an, 2:103)

Katika tamko hilo, amri ya kumcha Mwenyezi Mungu na kufa Muislamu inaelekezwa kwa Waumini, hivyo kuonyesha jinsi Uislamu unavyoweka umuhimu mkubwa, si tu katika maisha mazuri, bali pia kifo kizuri. Katika mazingira hayo, Waumini wanaonywa dhidi ya kubweteka, hali inayoweza kuwapeleka kwenye mwisho mbaya. Watu wengi wanajaribu kukwepa kuzungumzia kifo, licha ya ukweli kwamba kifo ni moja miongoni mwa vitu ...

Read More »

Maisha Ya Hind Bint Utba

Kabla ya kusilimu Leo tunaendelea kuhadithia na kisa cha Swahaba Hind na mumewe Abuu Sufian bin Harb tulichokianza toleo lililopita ambapo tuliona kuwa kabla ya kusilimu, kwa muda usiopungua miaka 20, alitumia mali, vipawa na muda wake kuendesha uadui dhidi ya Uislamu. Tuliona pia miongoni mwa waliouawa katika Vita vya Badr ambavyo Waislamu licha ya uchache na uhaba wa silaha, ...

Read More »