Tag Archives: Qur’an

Tuzidishe Wema Siku 10 za Dhul-hijja

Tumo ndani ya siku 10 tukufu za mwezi wa Dhul-Hijja. Allah Mtukufu ameziapia siku hizi 10 ndani ya kitabu chake kitukufu cha Qur’an pale aliposema: “Naapa kwa alfajiri. Na kwa siku 10.” [Qur’an, 89:1-2]. Wanazuoni wengi wa tafsiri ya Qur’an wamesema kilichoapiwa katika aya hii ni siku 10 za mwanzo wa Dhul-Hijja, yaani Mfungo tatu, na mtazamo huu pia wameusema ...

Read More »

Maajabu ya Bismillah

‘Bismillah’ ni kalima (tamko) maarufu kwa kila Muislamu. Ni tamko la ufunguo ambalo hutumika kabla ya kuanza kufanya jambo lolote. ‘Bismillah’ ni neno la ajabu kwa kuwa limepenya na kutumika katika maeneo mengi sana. Jambo la kushangaza na pengine la kufurahisha ni kuwa, wapo Waislamu wengi ambao wameutupa mbali Uislamu wao, lakini, utawasikia kabla ya kula, au kuanza safari kwa ...

Read More »

Mdhukuru Allah Aibariki Nyumba Yako

Dhikri au kumtaja Allah ndiyo uhai na usafi wa nyumba ya Muislamu. Utekelezaji wa jambo hili ni kielelezo cha kufikia lengo la kuitakasa nyumba dhidi ya maadui na viumbe waovu. Kinyume chake ni kutomdhukuru Allah kunakopelekea shida na balaa ndani ya nyumba. Kuipenda na kuikumbatia dunia ni moja ya sababu inayowafanya wengi waghafilike na na ibada ya kumtaja Mwenyezi Mungu. ...

Read More »

Hakika Allah Anakuamrisheni Kuzirudisha Amana Kwa Wenyewe…

“Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni kuzirudisha amana kwa wenyewe. Na mnapohukumu baina ya watu mhukumu kwa haki. Bila shaka mawaidha anayokutoleeni Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye asikiaye na aonaye” (Qur’an, 4:58). Kama tulivyosema awali, ukiakisi kwa kina, utaona amana ina maana pana zaidi kuliko tunavyoweza kufikiri. Amana ipo katika kila kipengele cha maisha yetu. Hebu tuangalie mifano ...

Read More »