Tag Archives: Maisha ya maswahaba

Miongoni mwa Alama za Kiyama

Twariq [Allah amrehemu] amehadithia kuwa, walikuwa wamekaa kwa Abdullah bin Mas’oud [Allah amridhie]. Mara muadhini wake akaja, akasema: “Qad qaamati Swalaa” akiwatanabahisha kuwa ni wakati wa Swala. Ibnu Mas’oud(ra) alisimama, nao wakasimama pamoja naye, wakaingia msikitini. Akawaona watu wamerukuu; akatoa takbira halafu akarukuu. Nao wakaenda na kufanya alivyofanya. Wakati wanaswali, akapita mtu mmoja kwa haraka, akasema: “Amani ikushukie Abuu AbdirRahman,” ...

Read More »

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy, Maisha yake baada ya kusilimu

Kutokana na maelezo yaliyotangulia tunajifunza kwamba Salmaan alisilimu mwaka wa kwanza Hijriya mara tu baada ya Mtume [rehema za Allah na amani zimshukie] kuwasili Madina. Kuanzia hapo aliishi na Mtume na inasemekana alikuwa muachwa huru wake, kwa maana Mtume alimlipia gharama za kumkomboa. Na pia Salmaan anatajwa kuwa ni katika watu aliyowapa hadhi yakuwa mtu wa nyumbani mwake [Ahlu bayti]. ...

Read More »

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy (as) -2

Kutoka katika kitabu,‘Suwarun min hayati swahaba,’ Salmaan Alfarsiy, Swahaba mtukufu, anaendelea kusimulia, kuwa baada ya kuishi Ammuuriya na mwalimu wake muda aliojaaliwa, ulifika muda wa mwalimu kuiaga dunia. Salmaan Alfaarisy (Allah amridhie) alimuuliza: “Unaniusia nini baada ya wewe kuondoka?” Mwalimu wake akamjibu: “Sidhani kama kumebaki mtu yoyote juu ya mgongo huu wa ardhi aliyeshika dini sahihi hii tuliyoishika sisi. Lakini ...

Read More »

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy (Allah amridhie)

Wiki hii tunaanza kumzungumzia Swahaba aitwaye Salmaan al-Faarisy. Huyu ni Swahaba aliyepata umaarufu mkubwa nakupendwa sana na Waislamu kuanzia wakati wa Mtume hadi leo hii. Salmaan ambaye alitokea Fursi, (Iran ya leo), alipewa jina la ‘Assaii waraal haqiqa’ (mwenda nyuma ya haki). Jina la Salmaan kabla ya kusilimu lilikuwa ni Ruuzba bin Jashbuudhan. Ni Swahaba huyu ndie aliyeshauri Waislamu wachimbe handaki ...

Read More »