Fahamu usyoyajua

Canada Lynx: Paka anayehimili kuishi kwenye baridi

Ndugu yangu msomaji, hakika Allah, Mbora wa Uumbaji ana Utukufu wa hali ya juu. Utabaini hilo ukitazama viumbe mbalimbali alivyoviumba katika ulimwengu wake huu. Juma hili tumtazame mmoja wa viumbe wa Allah, jamii ya paka aitwaye ‘Canada lynx’.
Huyu ni paka mkubwa kiasi anayepatikana Amerika ya Kaskazini katika nchi za Canada na Marekani. Paka huyu mwenye manyoya mengi na marefu anafahamika pia kwa jina la kisayansi la ‘Lynx canadensis’. Masikio yake yana umbo la pembe tatu na kwa juu yana vinywele virefu vyenye rangi nyeusi.

Pia ana masharubu marefu, miguu mirefu na mkia mfupi sana kiasi kwamba unaweza kudhani umekat-wa lakini si hivyo bali ndiyo maumbile yake. Maeneo ambayo canada lynx hupendelea kuishi ni kwenye misi-tu minene; na huko ndiko wanakopatikana sungura kwa wingi ambao ndiyo chakula chao pendwa.

Ndugu yangu msomaji, tambua Allah ‘Azza Wajallah’ ameumba viumbe mbalimbali kulingana na mazingira wanayoishi, ndiyo maana utashangaa kuna viumbe wen-gine wanahimili kuishi sehemu zenye joto na wakipele-kwa sehemu zenye baridi hawawezi kuishi; na wengine (akiwemo huyu canada lynx) wanahimili sehemu zenye baridi na wakipelekwa sehemu zenye joto hawawezi kuishi.

Urefu wa canada lynx kuanzia kichwani hadi miguuni ni kati ya sentimita 48 hadi 56 na uzito wake unaanzia kilogramu tano hadi 17. Pia, paka huyu ana meno 28. Allah, Mbora wa Uumbaji na anayejua kukadiria ame-jaalia umri wa kuishi wa canada lynx kuwa ni miaka 15.

Chakula na uzazi Wataalamu wa elimu ya viumbe wanasema, canada lynx ni katika viumbe wanaokula nyama (carnivorous). Wanyama hawa pia hupendelea sana kuwinda sungura wa barafu na mamalia wengine wadogo, hasa nyakati za usiku. Na ikitokea wamekosa kabisa chakula hula mizoga ya wanyama wadogo. Kwa upande wa uzazi, canada lynx anazaa na kunyo-nyesha. Kwa kawaida, canada lynx huzaa watoto kuanzia mmoja hadi nane; na akishazaa ananyonyesha watoto wake kwa muda wa majuma 12. Canada lynx pia ni katika viumbe ambao wana kipindi maalum cha kupandana, ambacho ni mwezi Machi hadi Aprili.

Mambo 10 usiyoyafahamu kuhusu canada lynx

Mosi, paka hawa wameumbwa kwa namna ambayo wanaweza kuakisi mazingira waliyopo kwa maana ya kuhimili baridi. Hapo ndiyo utaona uhodari wa Allah katika kuumba.
Pili, paka hawa hujiwekea akiba ya chakula baada ya kushiba kwa ajili ya matumizi ya baadae.
Tatu, kupungua na kuongezeka kwa wanyama hawa kunategemeana sana na wingi wa sungura. Sungura wakipungua, nao wanapunguza kuzaa. Kadhalika, sun-gura wakiwa wengi, nao huzaliana kwa wingi.
Nne, inasemekana canada lynx wanaweza kufugwa. Inaelezwa kuwa, wapo watu huko Marekani na Canada wanaowafuga kama paka wa nyumbani.
Tano, maadui wakubwa wa canada lynx ni binadamu, ambao huwawinda ili kupata ngozi yao. Jambo jema ni kuwa, hivi sasa kuna sheria za kuwalinda wanyama hawa.
Sita, licha ya kuwa na miguu mirefu, canada lynx hawezi kutembea haraka (kwa kasi). Hata anapomu-winda mnyama, humnyatia mpaka pale anapomkaribia ndiyo humkamata.
Saba, ni mahodari wa kuogelea na kukwea miti.
Nane, madume ya paka hawa yanapenda kukaa peke yao. Tisa, canada lynx ni mahodari sana katika kuwinda nyakati za usiku, labda kwa sababu uwindaji wao ni wa kunyatia.
Kumi, mara nyingi canada lynx akifanikiwa kumka-mata sungura anambana kichwani kwa mdomo wake na kisha anarudi naye kule alikotoka tayari kwenda kumla.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button