1. Afya

Kwanini tunahimizwa kula daku?

Kula daku ni jambo lililokoko- tezwa sana na Uislamu kama tunakavyo ona katika Aya na Hadithi za Mtume Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie) katika makala hii.

Qur’an na daku “

. . . Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajir katika weusi wa usiku. . . ” (Qur’an,2:187). Ayahiiinatuhimi- za kula na kunywa mpaka karibu na Alfajir. Hiki chakula kinacholi- wa usiku wa manane kwa ajili ya kujiandaa kufunga siku inayofuata ndiyo kwa kiswahili kinaitwa daku. Pia, daku kinaweza kuwa kinywaji kinachotumika usiku wa manane kwa ajili ya kufunga siku inayofua- ta.

Sunna na daku

Muhimu kula daku na kuchelewa kula daku. Mtume (re- hema na amani ya Allah zimshukie) alikuwa anakula daku baada ya kia- si cha kusoma Aya 50 za Qur’an anaswali swala ya Alfajiri (makisio ni sawa na dakika 15 kabla ya swala ya Alfajiri). Mtume Muhamad (re- hema na amani za Mwenyezi Mun- gu zimfikie) amesisitiza sana kula daku. Daku na kurehemewa Kula daku vilevile ni miongoni mwa sunna tukufu zinazodharauli- wa na wengi kati ya waislam na fa- dhila zake ni kubwa kupita kiasi, miongoni mwazo ni kurehemewa na Allah na kutakiwa msamaha na Malaika Watukufu kama alivyose- ma Mtume (rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie) katika Hadithi: “Hakika Allah na Malaika wake wanawarehemu wenye kula daku.”(Twabrani, IbnuHabban). Daku ni baraka Mtume Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie) amesisitiza katika Hadithi nyingine kwa kusema: “Hakika daku ni baraka amekupeni Allah, hivyobasimsiiache,” (Nasai).

Aina ya daku

Mlo wa daku unaweza kuwa mlo wowote ule hata kama maji ya kunywa kama tunavyojifunza kati- ka Hadithi ambapo amesema Abu Said Khudriy (Allah amridhie): “Daku ni baraka kwa hiyo msiliache japokuwa kwa tunda la maji. Maa- na Mwenyezi Mungu na Malaika wake huwarehemu wanaokula daku” (Ahmad).

Daku inavyotutofautisha

Katika Hadithi nyingine Mtume Muhammad anasema: “Kuleni daku, kwani ipo baraka katika kula daku. Na tofauti ya fadhila ya funga zetu sisi na Ahlul Kitabu (Wayahudi na Wakristo) ni huko kula daku”.

Muda wa daku

Unaruhusiwa kula daku hadi Alfajiri kitambo kidogo kabla hu- jaanza kufunga. Na hata Muadhini akiadhini na kama una tonge au fundo la maji mdomoni usiliteme, bali kamilisha kulimeza kisha ndiyo uanze kufunga. Haya yamethibiti katika Sunna. Umar (Allah amridhiye) amesema: “Mtume Muhammad (rehema na amani ya Allah zimshukie) alikuwa na waadhini wawili; Bilali na Ibn Ummi Maktuum. Akasema, ‘Haki- ka Bilali anaadhini usiku (adhana ya mwanzo), basi kuleni na mnywe hadi aadhini Ibn Ummi Maktu- um,’” (Bukhari na Muslim).

Muda mzuri

Wakati wa kula daku huanzia nusu ya usiku (saa sita) mpaka kab- la ya kuchomoza Alfajiri kwa muda mchache. Haya ni kwa mujibu wa kauli ya Swahaba wa Mtume Zaid bin Thaabit (Allah amridhie): “Tu- likula daku pamoja na Mtume wa Allah (rehema na amani za Allah zimshukie) kisha akainuka kwenda kuswali (Alfajiri). Nikamuuliza, ‘ki- likuwepo kitambo gani baina ya ad- hana ya Alfajiri na huko kula daku?’ Akasema, ‘Kiasi cha kusoma Aya 50,’” (Bukhari na Muslim).

Daku inadharauliwa

Kula daku ni miongoni mwa Sunna Tukufu zinazodharauliwa na wengi kati ya Waislamu, lakini fadhila zake ni kubwa kupita kiasi. Miongoni mwa faida hizo ni kure- hemewa na Allah na kutakiwa msa- maha na Malaika Watukufu kama

alivyosema Mtume Muhammad (rehema na amani ya Allah zimshukie) katika Hadithi: “Haki- ka Allah na Malaika wake wana- warehemu wenye kula daku,” (Twa- brani, Ibnu Habban).

Makundi ya vyakula

Vyakula vinaweza kugawanywa katika makundi makuu mawili kwa kigezo cha muda wake wa kukaa tumboni. Kundi la kwanza ni vyakula vinavyochukua muda mfupi, saa tatu mpaka nne ku- sagwa. Mfano wa vyakula hivyo ni vile laini kama ndizi, viazi na vile vi- tamu (tende, matunda). Kundi la pili la vyakula ni vyakula vinavyokaa tumboni kwa muda mrefu (kiasi cha saa 6 au zaidi). Mfano wa vyakula hivyo ni nafaka na mbegu – ngano, shahiri, mtama, mahindi, mchele na maharage.

Inashauriwa na wataalamu wa vyakula wa Kiislamu kuwa vyakula kama hivi viliwe kama daku au usikusanakwawalewanaoshindwa kuamka na kula daku. Vyakula hivi vitawapa nguvu ya kuhimili mikiki mikiki ya swaumu mchana na pia wataweza kumudu majukumu mengineyakazizamchana. Kwa hiyo, vyakula hivi ndiyo vizuri zaidi kuliwa kama daku. Funga siyo adhabu Katika funga nia kubwa ya Mwenyezi Mungu ni kupima utii wetu kwake, siyo kutukomoa. Ndi- yo maana funga ya Kiislamu ina- himiza kula daku karibu na Alfajiri na kutufuru mara tu jua linapo zama. Maana yake hizo ni takriban saa 14 (kati ya saa 24 za situ nzima). Hizi zinatosha kupima utii wetu kwa Mola. Hata hivyo, baadhi ya nchi kama Denmark huko Ulaya, kwa mwaka huu wa 2017 Waisla- mu wanafunga kwa saa 21. Yaani wanakula kwa saa 3 tu. Ingawa baadhi ya watu wanabeza na kudai kuwa sisi Waislamu tunakula Al- fajiri, halafu ndiyo tunafunga. Wa- jaribu na wao kufunga japo kwa saa 12 tu, achilia mbali saa 21 za Den- mark wataona ugumu wa swaumu, hasa kwa asiyefunga kwa imani ya kumkubali Mola. Huyu anaweza kusikia adha ya kuumwa kichwa na kutaka apewe dawa ya kutuliza mauimivu.

Show More

Related Articles

Close
Close