Latest

Mwinyi Ahimiza Maimamu Wawe Waliohifadhi Qur’an

Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muugano wa Tan- zania, Ali Hassan Mwinyi ame- shauri kuwa maimamu katika misikiti nchini wawe ni watu walio- hifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mun- gu, Qur’an Tukufu. Mzee Mwinyi alitoa ushauri huo wakati wa mashindano ya usomaji Qur’an yaliyoandaliwa na Taasisi ya al-Manahil Irfani Islamic Centre na kufanyika kwenye uwanja wa PTA Saba saba Temeke, Dar es Salaam. Aidha Mzee Mwinyi aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo aliwahimiza wazazi waongeze bidii katika kuwapeleka watoto wao madrasa kujifunza Uislamu, ikiwemo Qur’an, kwa faida ya mai- sha ya dunia na akhera ya watoto hao. Kadhalika, Mzee Mwinyi alisema hategemei kuona vijana hao waliohi- fadhi maneno ya Mwenyezi Mungu, Qur’an wakijiingiza katika tabia mbaya. “Ni muhimu kwa wazazi kuhak- ikisha wanawapelekea watoto wao madrasa, kwani huko ndiko wataka- pojifunza Qur’an kwa ufasaha,” alise- ma Mzee Mwinyi. Pia, Rais Mstaafu Mwinyi alihimiza kuendelea kufan- yika kwa mashindano ya usomaji Qur’an katika sehemu mbalimbali za nchi hii. Licha ya Mzee Mwinyi, mashindano hayo pia yalihudhuriwa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika serikali ya awamu ya nne, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Akizungumzakatikamashindano hayo, Mwenyekiti wa al-Manahil Ir- fani Islamic Centre, Soud Mussa Soud, taasisi iliyoandaa mashindano hayo amehimiza wazazi kupeleka watoto wao madrasa. “Wazazi wa- hakikishe wanawapeleka watoto wao madrasa. Leo hii tumeona wa-toto wadogo sana wamehifadhi Qur’an, jambo ambalo linatia hama- sa,” alisema Soud. Kwa upande wake, Naibu Katibu wa Taasisi hiyo, Ismail Hausi Mawe, aliwashukuru watu wote waliofanik- isha mashindano hayo. “Sisi kama taasisi tunapenda kuwashukuru wale wote waliohudhuria na kufani- kisha mashindano haya, na tuna- wasihi wadau wazidi kutuunga mkono,” alisema Mawe. Katika mashindano hayo, vijana wa umri mbalimbali walishindana kusoma Qur’an katika makundi manne ya wasomaji wa juzuu 10, ju- zuu 20, juzuu 25 na juzuu 30. Pia kulikuwa na kundi maalumu la wa- toto wa umri mdogo walioshindana katika juzuu moja. Washindi watatu katika kila kila kundi walikabidhiwa zawadi za fed- ha taslimu huku mshindi wa juzuu 30, Juma Khamis Suleiman, alikabi- dhiwa kitita cha shilingi laki Sita.

About Admin