Hapa na Pale

Rais Samia apongezwa Mkutano wa Nishati Afrika

Rais Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa ufanisi uliopatikana katika tukio la Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati Afrika (Mission 300) mwaka 2025.

Miongoni mwa taasisi zilizopompongeza Rais Samia ni Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania lililopitisha azimio la kumpogeza kwa kusema mkutano huo umeiletea sifa ya kipekee Tanzania na kutaja namna Watanzania walivyonufaika.

Akisoma azimio la pongezi hizo bungeni jana, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Asia Halamga, alisema mkutano huo ulikuwa na manufaa makubwa  kwa uchumi wa Tanzania na Bara zima la Afrika.

Halamga alisema wawekezaji katika sekta ya hoteli na malazi, usafiri na usafirishaji, wauzaji wa vyakula na vinywaji, wauzaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na sekta ya utalii wamenufaika huku baadhi ya wafanyabiashara wakitegeneza mtandao kwa kufanya mazungumzo ya kibiashara pembezoni mwa mkutano huo .

Alisema pia alisifu maazimio na ahadi za mipango ya mageuzi makubwa ya nishati mbadala na jadidifu, kuboreshwa kwa gridi za umeme na kuimarisha upatikanaji wa suluhu ya nishati safi za kupikia.

Pia alisema kuzinduliwa kwa Mipango ya Kitaifa ya Nishati kwa lengo la kuvutia wawekezaji na mageuzi ya sera; kutolewa kwa ahadi za ufadhili kutoka taasisi za kifedha za kimataifa kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Dunia. Moja ya mafanikio makubwa ilikuwa ni kupitishwa Azimio la Dar es Salaam likilenga kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa watu milioni 300 barani Afrika ifikapo 2030,  kuunganisha nishati kati ya nchi za Afrika, kutumia vyanzo vya nishati jadidifu kama jua, upepo, umeme wa maji, nishati za joto ardhi, ili kuwa na mifumo imara ya nishati.

Wageni takribani 2,600 wakiwamo wakuu wa serikali na nchi takribani 21 kutoka barani Afrika, mawaziri na viongozi mbalimbali wataasisi za kimataifa za fedha na nishati na wadau wengine walihudhuria mkutano huo.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button