Hapa na Pale

Rais Mwinyi ataka uadilifu katika biashara mwezi wa Ramadhan

Zikiwa zimebaki wiki tatu kuelekea mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza wafanyabiashara kufanya biashara kwa uadilifu na kuwa na huruma kwa wananchi.

Rais Mwinyi ametoa kauli hiyo Ijumaa wakati akizungumza katika Masjid Jibril Mkunazini, mjini Zanzibar alipojumuika katika ibada ya sala ya Ijumaa.

Alisema, kumekuwa na kawaida na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bei za bidhaa ufikapo mwezi wa Ramadhan, jambo ambalo si katika wema.

Rais Mwinyi alifahamisha kuwa Serikali imekuwa ikipunguza ushuru wa bidhaa katika Mwezi wa Ramadhan hivyo si jambo jema kwa wafanyabiashara kupandisha bei na kuwaongezea mzigo wananchi. Akizungumzia suala la Uchaguzi Mkuu ujao, Rais Mwinyi amewasisitiza Waumini Waislamu na wananchi kwa ujumla kudumisha amani ili uchaguzi huo ufanyike kwa utulivu na amani.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button