Habari

Wekezeni katika makuzi bora ya watoto

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, ameitaka jamii kuhakikisha kwamba wanafanya juhudi kubwa za kuwekeza kwenye makuzi na malezi  bora kwa watoto ili kuepuka taifa kuaribikiwa na vijana kimaadili.

Mhe. Othman ameyeyasema hayo huko msikiti wa Ijumaa uliopo Mtegani Makunduchi  Mkoa wa Kusini Unguja alipowasalimia waumini wa Kiislamu baada ya kukamilisha ibada ya swala ya Ijumaa alipoungana nao kwenye msikiti huo.

Amesema kwamba   jamii ya Wazanzibari hivi inaendelea kuelekea  kuharibikiwa kimaadili  kwa kuwa vijana wengi wanafuata na kuiga mila za kigeni jambo ambalo linachangiwa na wazazi kutokujitadi katika kuwekeza kwenye ulezi bora  na makuzi sahihi kwa  watoto ndani ya jamii.

Amefahamisha kwamba imani  na uislam kwa wazanzibari inaharibika kutokana na jamii na hasa wazazi kukosa kuwekeza vyema kwa vijana ambao ndio wanaokuja baadae na kwamba iwapo akukuzwa na maadili mema itokuwa vikumu kujakuyapata baadae.

Amesema ni vyema  kwa jamii kuendelea kujikita katika mambo ya maadili mema na kuyapanga sasa kwa kuwalea vyema vijana ili Zanzibar iweze kuendelea na historia njema ya hulka na maadili bora ya uislamu ambapo hata wagezi waliotembelea Zanzibar waliijua Zanzibar ni nchi tukufu iliyogubikwa na tabia na akhalaki njema za uislamu .
Amefahamisha kwamba hata watawala wa kikoloni waliweza kubariki taratibu na kuiridhia baadhi mila na kufuata na kushiriki katika kulinda mila za wazanzibari na pia wakapitisha sheria za kulinda mila ikiwemo ya kuzuia pombe kali.

Aida alisema kwamba katika kumbukumbu za kihistori zinaonesha kuwepo kesi maarufu  kati ya Mjerumani na Muingereza  ambao ulikuwa mgogoro wa ardhi iliweza kuamuliwa kwa kutumia sheria za kiislamu ambayo ndio iliyokuwa sheria mama ya Zanzibar  na wote waliridhia kutumika kwa sheria hiyo kwa kuwa wazanzibari wenyewe ndio walitumia na kujengeka kwa maadili ya sheria hizo.

Naye Khatib wa Swala ya Ijumaa Sheikh Haroub Sose amewataka waislamu na jamii kwa jumla nchini kuacha kufanya mambo maovu na kuiheshimu  miezi minne mitukufu ya mfunguo pili, tatu na mfunguo nne na mwezi huu wa Rajab kutokana na kuwa na matukio muhimu ya uislamu.

Mapema Mhe. Othman aliungana na waumini, ndugu, jamaa na wanafamilia kuzuru makaburi ya baadhi ya, Masheikh, wanazuoni na   watu mashuhuri  huko Makunduchi kuwaombea dua  akiwemo Sheikh Idrissa Abdulwakili, Sheikh Hassan Bin Ameir, Shekh Ali Haji Pandu na Sheikh Mamoud Kombo. 
Mwisho

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari leo Ijumaa Januari 17, 2025.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button