Walimu wa shule ya msingi Imaan na secondari Forest Hill wapatiwa mbinu za ufundishaji bora
Wito huo umetolewa na Sheikh Abdi Kassim Jiba wakati akiwasilisha mada ya sifa za mwalimu bora katika uislamu na athari zake kwa wanafunzi kwa mujibu wa Qur’an na sunnah katika semina ya walimu wa shule ya sekondari Forest Hill na shule ya Msingi Imaan English Medium School zinazomilikiwa na Taaasisi ya The Islamic Foundation ya Mjini Morogoro.
Aidha Sheikh Abdi Kassim Jiba ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) ameongeza kuwa sifa za mwalimu bora ni yule mwenye ikhlasi katika kazi yake.
Kadhalika Sheikh Abdi Jiba amewataka walimu hao kuwafundisha watoto kujiepusha na vitendo vya israfu.
Naye kiongozi wa shule za Forest Hill na Imaan Sekitya Ramadhan amesema kuwa ni matarajio yake kwamba mafunzo hayo, walimu watakwenda kuyafanyia kazi kwa moyo mmoja.
Nao washiriki wa semina hiyo ambao ni walimu wa shule za Forest Hill na shule ya Msingi Imaan wamesema kuwa semina kama hizo ziwe endelevu kwani zinawakumbusha kufanya kazi kwa kuzingatia miiko ya taaluma zao na kufuata kitabu cha Qur’an na sunnah za Mtume Muhammad S.A.W
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Imaan Salim Bahanzika amesema semina hiyo itawafanya walimu kuzingatia na kujali taratibu za ufundishaji kwa wanafunzi wao ili wanafunzi kuwa wastaarabu na wenye kujipamba na tabia njema.