Habari

Mwinyi: Sera ya uchumi wa buluu kutekelezwa kisayansi

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kui-tekeleza kisayansi sera ya uchumi wa buluu, hivyo itaweka nguvu katika tafiti za rasilimali za bahari.
Dk Mwinyi amesema hayo jana wakati uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la taaluma na utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari (IMS) inayojengwa chini ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dk Mwinyi alisema tukio hilo linafanyika katika sherehe za miaka 61 za Mapinduzi ya Zanzibar, hivyo SMZ itaendelea kutoa ush-irikiano.

“Sera yetu kuu ni sera ya uchumi wa buluu ambayo ndani yake kuna sekta ya utalii, uvu-vi, ukulima wa mwani na nyingine kadhaa, hivyo taasisi hii ina umuhimu wa pekee, itatu-patia wataalamu kwenye sekta mbalimbali za uchumi wa buluu.”

“Matarajio yetu chuo hiki kitatupatia matokeo ya tafiti mbalimbali zinazofanywa katika uchumi wa buluu. Kwa kuwa sera yetu ni uchumi wa buluu tunataka kuwa na sera zin-azotokana na matokeo ya kisayansi ili kuten-geneza sera zitakazoleta maendeleo,”alisema Mwinyi.

Mkuu wa UDSM, Rais mstaafu Jakaya Kik-wete alitoa shukrani kwa Serikali zote mbili kwa kuwezesha ujenzi huo. “Bila uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kukubali taasisi ya IMS iingizwe kwenye mra-di wa HEET tusingefika hatua hii, haikuwa rahisi kujumuisha taasisi hii kwenye mradi huu.

Ilibidi kwenda kuiona mamlaka nika-zungumza na Rais Samia akaniambia nisiwe na wasiwasi, taasisi ikaingia kwenye mradi. “Tunashukuru pia, uamuzi wa busara wa Rais Mwinyi uliotuwezesha kupata hati miliki ya ardhi ya eneo hili la Buyu. Bila uamuzi wa Rais nafikiri hadi sasa jambo hili lingeku-wa halijakamilika maana limechukua miaka mingi,” alisema Kikwete.

Alisema kwa mujibu wa utaratibu wa Benki ya Dunia, fedha za ujenzi zisingeweza kutole-wa kama Serikali haina hati miliki ya ardhi ya eneo husika.

“Ilitubidi tutafute hati katika maeneo yote ambayo tunajenga kampasi kwa kufuata taratibu, tulipozipata ndipo tukapeleka kwa wakubwa, Benki ya Dunia wakatupatia fedha hatimaye ujenzi ukaanza,” alisema Kikwete. “Binafsi najituma sana kuhakikisha nasi-mama kikamilifu kwenye kazi yangu ya ukuu wa chuo, wenzangu waliniamini wakanipa jukumu hili kwa sababu nisipofanya hivyo, wataona kama sichukulii kwa umakini.” Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alisema katika mra-di wa HEET kampasi mpya 16 zinajengwa mikoa 16 nchini ili kusogeza elimu ya juu.

Profesa Mkenda alivielekeza vyuo vikuu na kampasi zinazoanzishwa kutoa shahada za mafunzo ya kazi ili kuwezesha wahitimu wengi kujiajiri ikiwa ni sehemu ya jitihada na changamoto ya ukosefu wa ajira.Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Muhamed Mussa alisema mitalaa ya elimu ya SMZ kuanzia ngazi ya msingi na sekondari imeandaliwa kuhakikisha inawatengeneza wanafunzi wenye sifa za kujiunga katika vyuo vya uvuvi na sayansi za bahari ili wawe na ushiriki imara kwenye uchumi wa buluu.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button