
Maimam chini ya taasisi ya The Islamic Foundation watakiwa kuhubiri amani
MWENYEKITI wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi amewataka maimam walio chini ya Taasisi hiyo kuwa mabalozi wazuri wa kudumisha amani hasa katika kipindi hichi ambacho nchi inaeelekea katika uchaguzi mkuu
Mwenyekiti Aref amesema hayo wakati akifungua semina ya siku mbili kwa maimamu na walimu wa dini ya Kiislam iliyoanza leo Tarehe 25,02.2026 inayofanyikia mjini Morogoro ambapo amesema kuwa nafasi ya viongozi hao wa dini katika kudumisha amani ni kubwa

Ameongeza kuwa Taasisi hiyo itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kufundisha mafundisho sahihi ya dini ya Kiislam ambapo yamehimiza suala la amani kwa watu wote
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Islamic Foundation Sheikh Ibrahim Twaha amesema kuwa idara ya Daawa ndiyo idara yenye thamani kubwa katika taasisi hiyo hivyo kuwataka maimam hao kutokata tamaa katika kufikisha mafundisho sahihi ya dini kwa wamaumini wao
Kwa upande wao watoa mada katika Semina hiyo Sheikh Salim Bafadhili kutoka Tanga pamoja Sheikh Hassan Ahmed kutoka Mombasa nchini Kenya wamesema kuwa mada watakazozitoa zitasaidia maimam hao kuweza kupiga hatua zaidi katika kutoa daawa
nao Baadhi ya maimam na walimu walio chini ya Taasisi ya The Islamic Foundation licha ya kuishukuru Taasisi hiyo kwa kuwaleta pamoja wamesema kuwa elimu watakayoipata itawapa mbinu zaidi za ulinganiaji wa dini ya Kiislam






