
Bwawa la Kidunda kumaliza tatizo la maji Dar Es Salaam
Mradi mkubwa wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda linalojengwa Mkoani Morogoro litakuwa na uwezo wa kuhifadhi zaidi ya lita Bilioni 190 za maji na kugharimu kiasi cha shilingi Bilioni 336, umefikia zaidi aslimia 27 za utekelezaji wake ambapo mara baada ya kukamilika litasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Akizungumza katika ziara ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) waliotembelea ujenzi wa mradi huo kwa lengo la kujionea hatua iliyofikia ya utekelezaji, Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Bwire Mkama amesema kuwa Jiji la Dar es salaam limekuwa likikutana na changamoto ya upatikanaji wa maji hususani kipindi cha kiangazi hivyo kukamilika kwa Bwawa la kidunda litakwenda kumaliza kabisa changamoto na kuboresha huduma ya majisafi na salama.
Awali, Meneja Sehemu ya Mazingira na uratibu wa Jumuiya za watumia maji kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Bi. Janeth Kisoma amebainisha kuwa Bwawa la kidunda ni miongoni mwa vyanzo vya maji vinavyosimamiwa na Wami/Ruvu huku akieleza mipango iliyopo ya kulitangaza kuwa eneo tengefu.
Aidha, Bi. Janeth amesema kuwa Bodi imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika kuhifadhi mazingira ambapo mpaka sasa zaidi ya Mabiriki 29 ya kunyweshea mifugo yameshajenga kwenye vijiji vinavyouzunguka Mto Ruvu ili mifugo is isiweze kuingia mtoni na kuharibu chanzo hicho cha maji.
“Tonelamajilazimalihifadhiwe “




