Wema Waliotangulia

Tujifunzayo katika maisha ya Salmaan bin Alfaarisy MAISHA YA MASWAHABA: 4

Tunapoipitia sira ya kila Swahaba katika Maswahaba wa Mtume, tunakuta maajabu na mazingatio makubwa yanayogusa maisha yetu kiimani, kifamilia, kiutamaduni na kijamii. Hata hivyo, safari ya Maswahaba ya kuitafuta neema ya Uislamu hutofautiana sana. kwa mfano, safari ya kuufikia Uislamu ya Maswahaba kama vile Abubakr, Uthman, Ali, Abdurahman bin Auf zilikuwa fupi sana, lakini safari ya Swahaba Salmaan [Allah amri- ...

Read More »

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy, Maisha yake baada ya kusilimu

Kutokana na maelezo yaliyotangulia tunajifunza kwamba Salmaan alisilimu mwaka wa kwanza Hijriya mara tu baada ya Mtume [rehema za Allah na amani zimshukie] kuwasili Madina. Kuanzia hapo aliishi na Mtume na inasemekana alikuwa muachwa huru wake, kwa maana Mtume alimlipia gharama za kumkomboa. Na pia Salmaan anatajwa kuwa ni katika watu aliyowapa hadhi yakuwa mtu wa nyumbani mwake [Ahlu bayti]. ...

Read More »

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy (as) -2

Kutoka katika kitabu,‘Suwarun min hayati swahaba,’ Salmaan Alfarsiy, Swahaba mtukufu, anaendelea kusimulia, kuwa baada ya kuishi Ammuuriya na mwalimu wake muda aliojaaliwa, ulifika muda wa mwalimu kuiaga dunia. Salmaan Alfaarisy (Allah amridhie) alimuuliza: “Unaniusia nini baada ya wewe kuondoka?” Mwalimu wake akamjibu: “Sidhani kama kumebaki mtu yoyote juu ya mgongo huu wa ardhi aliyeshika dini sahihi hii tuliyoishika sisi. Lakini ...

Read More »

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy (Allah amridhie)

Wiki hii tunaanza kumzungumzia Swahaba aitwaye Salmaan al-Faarisy. Huyu ni Swahaba aliyepata umaarufu mkubwa nakupendwa sana na Waislamu kuanzia wakati wa Mtume hadi leo hii. Salmaan ambaye alitokea Fursi, (Iran ya leo), alipewa jina la ‘Assaii waraal haqiqa’ (mwenda nyuma ya haki). Jina la Salmaan kabla ya kusilimu lilikuwa ni Ruuzba bin Jashbuudhan. Ni Swahaba huyu ndie aliyeshauri Waislamu wachimbe handaki ...

Read More »

MAISHA YA HINDU BINT UTBAH, MKE WA ABUU SUFIANI

K ama ilivyo kawaida, kutoka katika maisha ya wema waliotangulia ambao visa vyao tunavisimulia hapa tunajifunza humo mambo mengi ya kutunufaisha. Katika maisha ya Hindu bint Utba (radhi za Allah zimshukie) Waislamu wana mengi ya kujifunza. Miongoni mwa hayo, kubwa zaidi ni kuwa kisa hiki kimethibitisha ukweli wa maneno ya Mtume (rehema na amani zimshukie) aliposema “Nyoyo za waja zimo ...

Read More »

Maisha Ya Hindu Bint Utbah, Mke Wa Abuu Sufiani

Msimamo wake mbele ya Mtume Hindu baada ya kusilimu alikwenda kwa Mtume na kuudhihirisha msimamo wake kwa kusema: “Ewe mjumbe wa Allah, Wallahi hawakuwepo watu ninao wachukia na kuwatakia kila baya liwafike kuliko wafuasi wako, lakini nashangaa sasa kuwa hakuna katika mgongo wa ardhi watu niwapendao na kupenda Allah awape heshima kuliko wafuasi wako.” Mtume alifurahi na kumwambia: “Na ndivyo ...

Read More »

Maisha Ya Hind Bint Utba

Kabla ya kusilimu Leo tunaendelea kuhadithia na kisa cha Swahaba Hind na mumewe Abuu Sufian bin Harb tulichokianza toleo lililopita ambapo tuliona kuwa kabla ya kusilimu, kwa muda usiopungua miaka 20, alitumia mali, vipawa na muda wake kuendesha uadui dhidi ya Uislamu. Tuliona pia miongoni mwa waliouawa katika Vita vya Badr ambavyo Waislamu licha ya uchache na uhaba wa silaha, ...

Read More »

Tujifunzayo kutoka maisha ya Asmaa bint Umais

Wanaume kuingia katika majumba ya wengine bila ya nidhamu, kimaumbile na kisheria, ni jambo linalowakera sana waume na wazazi. Na hapa ndipo tunapogundua siri ya agizo lililokuja ndani ya Qur’an, (24:27) la kuwataka waumini wasiingie majumba yasiyo yao ila kwa rukhsa. Ukweli huu uko wazi katika sira ya Asmaa pale Abubakr kununa (kuhisi wivu) baada ya kuwakuta jamaa fulani (wanaume) ...

Read More »