Tujikumbushe

Wala msife ila mmekuwa Waislamu (Qur’an, 2:103)

Katika tamko hilo, amri ya kumcha Mwenyezi Mungu na kufa Muislamu inaelekezwa kwa Waumini, hivyo kuonyesha jinsi Uislamu unavyoweka umuhimu mkubwa, si tu katika maisha mazuri, bali pia kifo kizuri. Katika mazingira hayo, Waumini wanaonywa dhidi ya kubweteka, hali inayoweza kuwapeleka kwenye mwisho mbaya. Watu wengi wanajaribu kukwepa kuzungumzia kifo, licha ya ukweli kwamba kifo ni moja miongoni mwa vitu ...

Read More »

Swala inahitaji maandalizi-4

Swala ya jamaa na umuhimu wake Moja ya malengo makuu ya kujengwa na kuwepo misikiti katika maeneo wanayoishi Waislamu ni kuwakusanya ili waswali pamoja, yaani swala ya jamaa. Swala ya jamaa maana yake ni watu kujumuika na kuswali pamoja nyuma ya imamu (kiongozi) mmoja wa ibada ndio maana Mtume akasisitiza kwamba, watu watatu au wawili tu wakiishi sehemu lazima waswali ...

Read More »

Swala inahitaji maandalizi -2

Kutokana na aya 29:45 katika Qur’an tuliyoitaja katika toleo lililopita na ambayo tutakuwa tukiirejearejea, tulijifunza kuwa,Swala ni nyenzo kubwa ya kumkinga mja na jamii kwa ujumla dhidi ya maovu na machafu. Pia, tuliona kwamba, kukingwa dhidi ya maovu, ndio haswa lengo la agizo la Muumba kwetu la kutekeleza ibada ya swala… Kazi kubwa inayomkabili kila Muislamu ni kujifunza falsafa iliyotumika ...

Read More »

Swala inahitaji maandalizi-3

Kabla ya kuelekea msikitini, inapendeza zaidi ukichukua udhu nyumbani. Msingi wa hili ni Qur’an. Allah Aliyetukuka anasema: “Enyi watu, chukueni mapambo yenu wakati wa kila swala, na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri) lakini msipite kiasi, hakika yeye (Mwenyezi Mungu hawapendi wapitao kiasi.” (Qur’an, 7: 32) Aya hii, licha ya kututaka tutumie neema na riziki, ikiwa ni pamoja na vyakula na ...

Read More »

Mipaka ya kuchukiana baina ya Waislamu

Kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allah [Al-walaa wal-baraa] Mpenzi msomaji, mlango wa kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allah (Al-walaa Wal-baraa) haujaishia kwa Waislamu na makafiri tu bali uko baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe. Ikiwa Muislamu ndani yake ana imani na maasia, basi atapendwa kutokana na imani yake na kuchukiwa kutokana na maasia yake. Hii iko hata katika ...

Read More »

FALSAFA YA SADAKA

Ulichotoa Kimebakia,ulichotumia kimemalizika Aisha (Allah amridhie) amesimulia kwamba walichinja mbuzi. Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) Akasema: “Kuna kilichobaki?” Akasema: “Hakuna kilichobakia isipokuwa bega lake.” Akasema (Mtume): “Mbuzi wote amebaki isipokuwa bega lake” (Tirmidhy, na al-Baaniy Amesema ni sahihi). Katika tukio hili tunajifunza umuhimu wa kujitolea na thamani ya kile alichokitoa mtu. Kwa kawaida, nafsi huona kama inapungukiwa pale ...

Read More »

Swala inahitaji maandalizi-1

Swala ni nguzo ya pili katika nguzo za kiislamu, na ni ibada kongwe iliyotekelezwa na Mitume wa zama zote pamoja na wafuasi wao. Swala pia ni kigezo kikuu cha ukweli wa Uislamu wa mtu. Kuitekeleza swala ni sababu ya kukingwa na adhabu ya moto huko Akhera, kupata radhi za Allah  na kuingizwa Peponi. Vile vile kuiacha Swala ndio sababu kuu ...

Read More »

Sema Bismillah Wakati Wa Kula

Hudhayfatu Ibnu Alyamaaniy [Allah amridhie] amesema: “Tulikuwa tunapohudhuria kwa ajili ya kula chakula pamoja na Mtume [rehema za Allah na amani zimshukie] hatuweki mikono yetu [katika sahani] mpaka aanze Mjumbe wa Allah kuweka mkono wake. Wakati fulani tulihudhuria pamoja naye kula chakula, akaja kijakazi mmoja kama vile amesukumwa [alikuwa mwenye haraka], akaenda kwa ajili ya kuweka mkono wake kwenye chakula, ...

Read More »

Maisha Na Itikadi Ya Sheikh Muhammad Bin Abdulwahhab;

Da’wah ya Sheikh Ibn Abdulwahhab (mwendelezo) Kazi ya da’wah ya Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab (Allah amrehemu) inajieleza yenyewe na inakanusha kila aina ya uongo na uzandiki dhidi yake. Miongoni mwa kazi alizozifanya ni kukata miti ambayo Waislamu wa Najd walikuwa wakiiabudu na kuiomba kwa itikadi zao mbali mbali, maombi ambayo yalipaswa kuelekezewa Allah Ta’ala pekee. Miti aliyoikata ilifanana na ile ...

Read More »

Maisha na Itikadi ya Sheikh Muhammad bin Abdulwahhab

Muhammad bin Abdulwahhab kama ‘Mujaddid’ Mujaddid katika katika dini ni mtu aliyekuja kurejesha upya dini kuwa kama vile ilivyokuwa zama za Mtume na Maswahaba. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Huraira (Allah amridhie) kwamba Mtume wa Allah (rehema na amani za Allah ziwe juu yake) alisema: “Hakika Allah hutuma kwa ajili ya umati huu katika mwanzo wa kila miaka mia moja ...

Read More »