Misk ya Roho

Nunueni tiketi ‘Misk ya Roho’ mapema kuepuka usumbufu

Ikiwa imesalia takribani wiki moja na nusu kufanyika kwa kongamano la pili la Misk ya roho hapa nchini, Waislamu wamehimizwa kukata tiketi mapema ili kuondokana na usumbufu wa kinyang’anyiro cha tiketi siku ya mwisho. Uzoefu wa makongamano yaliyopita unaonresha kuwa, baadhi ya watu waliosubiri kukata tiketi siku za mwisho walikosa tiketi na hivyo kujikuta wakijuta. Akizungumzia maendeleo ya mauzo ya ...

Read More »

Kipyenga cha Misk ya Roho 2018 Kimeshapulizwa…

Mada kuu: ‘Utukufu Wake…’ Katika muendelezo wa mfululizo wa makongamano mbalimbali yanayoandaliwa na taasisi ya The Islamic Foundation (TIF), kwa mara ya pili mtawalia tunawaletea kongamano kubwa kuwahi kutokea katika ukanda wa Afrika Mashariki litakaloendeshwa kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Misk ya Roho ni kongamano la kidaawah la Afrika Mashariki ambapo TIF, huwaalika masheikh kutoka katika nchi za Afrika ...

Read More »

MISKI YA ROHO TENA…

Salamu alaykumu, kipazani najongea. Ndugu zangu isilamu, ujumbe nawaletea. Miski tuliyoihamu, punde tu itatujia. Roho zipate nukia, miski inatulazimu. Uturi huu muhimu, TIF yatusogezea. Mashekhe walo adhimu, toka kwetu tanzania. Hata watokao lamu, burundi uganda pia. Roho zipate nukia, miski inatulazimu. Tusiwazie ugumu, ni nafuu nawambia. Shilingi si darahimu, elfu tano kuchangia. Tiketi kila sehemu, hata kwa simu lipia. Roho ...

Read More »

‘Kuihudumia Dini’ Na Sheikh Zuberi Bizimana

Sheikh Zuberi Bizimana ni mmoja kati ya Masheikh waliobahatika kuwasilisha mada katika kongamano la Misk ya roho lililofanyika Novemba 26, mwaka 2017 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Sheikh Bizimana alizaliwa huko Buyenzi nchini Burundi na kutokana na mapenzi yake ya kutafuta elimu ya dini alipata fursa ya kusoma katika chuo cha Muhammad Ibn Al-Saudi kilichopo Riyadh ...

Read More »

Kikao cha TIF Volunteers chafana

Wajipanga kongamano la Misk ya Roho 2018 Jumapili iliyopita ya tarehe 12 mwezi wa nane ilikuwa ni ya kipekee kwa volunteers wa taasisi ya The Islamic Foundation baada ya kufanya kikao cha kwanza cha kimkakati kuelekea kongamano la pili la Afrika Mashariki lijulikano kama Misk ya Roho 2018. Kikao hicho kilichowakutanisha pamoja volunteers wa zamani na wapya wa TIF kilifanyika ...

Read More »

Kwa ajili ya kupata Radhi za Allah

Umeshawahi kuwa katika sehemu ambayo umezungukwa na watu wengi lakini bado ukajihisi mpweke? Mara nyingine tunahisi kama kuna kitu kimekosekana na mara nyingine tunajilaumu kwa kuwa katika muda huo, mioyo yetu haihisi ukaribu na Allah. Unahisi pumzi kama vile imekuwa nzito na kuna maumivu katika roho yako. Katika njia rahisi za kutufanya tuhisi kama tunavuta pumzi safi na kupelekea kupata ...

Read More »

Umuhimu wa kuhudhuria kongamano la Misk ya Roho

Misk ya Roho ni Kongamano kubwa la kida’awah kuwahi kufanyika katika historia ya Tanzania. Ni Watanzania au wana Afrika Mashariki wa kawaida wachache sana wanaoweza kumudu kusafiri nchi mbalimbali za eneo hili kuhudhuria mihadhara na makongamano ili kustafidi na kupata ladha tofauti za masheikh wa nchi hizo. Hii ni kwa sababu za uchache wa kipato na muda. Hata hivyo, Kongamano ...

Read More »

Kumbukizi ya Misk ya Roho ya 2017

Mnamo Novemba 26, 2017, historia iliandikwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa kufanyika kwa kongamano kubwa la kwanza lililojumuisha masheikh mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki. Masheikh hao walikutanishwa katika jukwaa moja na kukonga nyoyo za Waislamu sio tu wa Afrika ya Mashariki bali duniani kote kwa ujumla ambao walifuatilia tukio hilo kupitia vyombo vya habari. Misk ya Roho ni ...

Read More »

Sheikh Kyebanja ashangazwa Watanzania kusifika kwa ushirikina

Featured Video Play Icon

“Ndugu zangu wa kutoka Tanzania nyie ni lazima mchunge sana. Mimi nimeishi Uganda na Kenya na huko kuna waganga wengi sana wanaojisifu kuwa wao ni wachawi kutoka Tanzania. Huko kwetu Uganda unaweza kukutana na mtu akakuambia ‘mimi usinichezee, mimi ni mganga kutoka Tanzania,”. Hayo ni maneno ya Sheikh Ibrahim Kyebanja aliyoyaongea katika kongamano la kwanza la Afrika Mashariki lililofanyika kwenye ...

Read More »

Mwenyekiti TIF aahidi makongamano mengine makubwa zaidi

Aref Nahdi, Mwenyekiti wa The Islamic Foundation (TIF) amesema kuwa taasisi yake inatarajia kuja na makongamano makubwa zaidi kwa ajili ya kutoa da’awa kwa Waislamu hapa nchini. Mwenyekiti Aref Nahdi aliyasema hayo kwenye kongamano la Misk ya Roho lililofanyika Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo alisema Waislamu wengi wameonesha hamasa kwenye kongamano la Misk ya roho na mengine, hivyo ...

Read More »