Kutoka Katika Quran na Sunnah

Sala ya Idd na hukumu za kuchinja (Udh-hiya)

Kutoka kwa swahaba Bara-a bin Azib, (Mwenyezi Mungu awe radhi naye), alihadithia kuwa Mtume (amani ya Mungu iwe juu yake), alipotoka kwenye siku ya Idd ya kuchinja, alianza na swala; kisha akatugeukia kwa uso wake, (na) akasema: “Ibada yetu ya kwanza katika siku hii tunaanza na kuswali, tukishamaliza swala tutakwenda kuchinja.” Mtume (saw) akaendelea kusema: “Kwa mtu aliyeswali pamoja nasi ...

Read More »

Tuzidishe Wema Siku 10 za Dhul-hijja

Tumo ndani ya siku 10 tukufu za mwezi wa Dhul-Hijja. Allah Mtukufu ameziapia siku hizi 10 ndani ya kitabu chake kitukufu cha Qur’an pale aliposema: “Naapa kwa alfajiri. Na kwa siku 10.” [Qur’an, 89:1-2]. Wanazuoni wengi wa tafsiri ya Qur’an wamesema kilichoapiwa katika aya hii ni siku 10 za mwanzo wa Dhul-Hijja, yaani Mfungo tatu, na mtazamo huu pia wameusema ...

Read More »

Maajabu ya Bismillah

‘Bismillah’ ni kalima (tamko) maarufu kwa kila Muislamu. Ni tamko la ufunguo ambalo hutumika kabla ya kuanza kufanya jambo lolote. ‘Bismillah’ ni neno la ajabu kwa kuwa limepenya na kutumika katika maeneo mengi sana. Jambo la kushangaza na pengine la kufurahisha ni kuwa, wapo Waislamu wengi ambao wameutupa mbali Uislamu wao, lakini, utawasikia kabla ya kula, au kuanza safari kwa ...

Read More »

Kudumu na ibada baada ya Ramadhani ni ishara ya kukubaliwa swaumu

Allah anasema; “Na Muham- mad si yeyote isipokuwa ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume. Je, akifa au akiuawa mtageuka nyuma ya visigino vyenu (mrudi ukafirini)? Na atakayegeuka nyuma ya visig- ino vyake, basi hatomdhuru Al- lah kitu chochote. Na Allah ata- walipa wenye kushukuru. Na unaelewa nini unaposoma Hadithi ya Mtume iliyorekodiwa na Imamu Bukhari na Muslim kutoka kwa ...

Read More »

Muislamu na swaumu

Katika Hadithi, Mtume wetu Muhammad (rehema na amani za Allah zimshukie) amesema; “Anaposafiri mja au kuugua huwa anaandikiwa thawabu za yale ambayo alikuwa na ada ya kuyafanya wakati akiwa hajasa- firi na mzima.” Wanawake wengi wanap- opatwa na ada zao za kimaum- bile ndani ya Mwezi wa Ramad- hani, hukata tamaa kwa kuche- lea na kuhofia kupitwa na kheri na ...

Read More »

Muislamu na swaumu

Allah anasema: “Enyi mlio- amini! Mmefaridhishwa kufun- ga (swaumu) kama ilivyofari- dhishwa kwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kuwa wachaMun- gu. (Swaumu ni) Siku za kuhesa- bika. Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safa- rini, basi akamilishe idadi katika masiku mengineyo. “Na kwa wale wanaoiweza la- kini kwa mashaka watoe fidia; kulisha masikini. Na atakayefan- ya kwa khiari yake ...

Read More »

muislamu na swaumu

“Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safa- rini, basi akamilishe idadi katika masiku mengineyo. Na kwa wale wanaoiweza lakini kwa mashaka watoe fidia; kulisha masikini. Na atakayefanya kwa hiyari yake jema lolote, basi hilo ni bora kwake. “Na mkifunga Swaumu ni bora kwenu mkiwa mnajua. Mwezi wa Ramadhani ambao imeterem- shwa humo Qur’an ili iwe muon- gozo kwa watu ...

Read More »

Sayansi Mamboleo Na Mafunzo Mbalimbali Ambatanishi

“Na lau kama hakuwa mion – goni mwa wenye kumsabbihi Al – lah. Angelibakia tumboni mwake mpaka Siku watakayofufuliwa (viumbe). Basi Tukamtupa kwenye ardhi tupu ufukweni (al – ipomcheua samaki) naye akiwa mgonjwa. Na Tukamuoteshea mti unaotambaa aina ya mung’unya. Na Tukamtuma kwa (watu wake) laki moja au wanaoz – idi. Wakaamini, basi Tuka – wastarehesha kwa muda,” (Qur’an, 37:139-148). ...

Read More »

Sayansi Mamboleo na Mafunzo Mbalimbali Ambatanishi

Imamu Bukhari anasimulia kutoka kwa Abu Huraira (Allah amridhie) kwamba Mtume Muhammad (rehema na amani ya Allah iwe peke yake) amesema: “Habbat-sawdaa inatibu kila kitu isipokuwa mauti.” Mpenzi msomaji, katika makala iliyopita nilikuahidi kuwa katika makala hii tutafahamishana juu ya baadhi ya magonjwa yanayotibiwa kwa asali. Kabla hatujaingia kuyataja baadhi ya magonjwa hayo hebu tutaje dawa nyingine muhimu iliyotajwa katika ...

Read More »

Sayansi Mamboleo na Mafunzo Mbalimbali Ambatanishi

“Na Mola wako alimtia ilhamu nyuki kwamba, jitengenezee nyumba katika majabali, na katika miti, na katika wanavyojenga (wanadamu). Kisha kula katika kila matunda, na fuata njia za Mola wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita). Kinatoka katika matumbo yao kinywaji cha rangi mbali mbali ndani yake mna shifaa (ya magonjwa) kwa watu. Hakika katika hayo, bila shaka ni Aya (ishara, dalili, zingatio) kwa ...

Read More »