Imaan Media

Jikinge na Bawasili Kwa Kubadili Mfumo wa Maisha

Bawasili ni moja ya magonjwa maarufu zaidi yanayoathiri mfumo wa chakula hususan njia ya haja kubwa. Wataalamu huita ugonjwa huu ‘hemorrhoids,’ jina ambalo limetokana na kuvimba na kuchomoza kwa mishipa ya damu inayopatikana katika puru (rectum) na mlango wa haja kubwa. Mishipa hii hujulikana kama ‘hemorrhoidal veins’ na kazi yake kubwa ni kusafirisha damu kwenda kwenye moyo na inaweza kuchomoza ...

Read More »

FALSAFA YA SADAKA

Ulichotoa Kimebakia,ulichotumia kimemalizika Aisha (Allah amridhie) amesimulia kwamba walichinja mbuzi. Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) Akasema: “Kuna kilichobaki?” Akasema: “Hakuna kilichobakia isipokuwa bega lake.” Akasema (Mtume): “Mbuzi wote amebaki isipokuwa bega lake” (Tirmidhy, na al-Baaniy Amesema ni sahihi). Katika tukio hili tunajifunza umuhimu wa kujitolea na thamani ya kile alichokitoa mtu. Kwa kawaida, nafsi huona kama inapungukiwa pale ...

Read More »

Mdudu Hatari Lakini Haumi

Msomaji wa Fahamu Usiyoyajua, juma hili ninakujuza tabia za mdudu aitwaye, ‘Nairobi Fly.’ Huyu ni jamii ya wadudu wanaopenda kuviringisha kinyesi, kwa Kiswahili ‘Tuta wale,’ kwa Kiingereza ‘Beettle’ lakini wadigo wanamuita Chidundu. Nairobi fly ana miguu sita; kulia mitatu na kushoto mitatu, lakini haruki. Pia, ana antenna mbili. Wadudu hawa, kwa mbele wana rangi nyekundu na nyeusi, na ukubwa wao ...

Read More »

Je, ni woga wa kawaida au ugonjwa wa wasiwasi? | Afya yako

  Ni jambo la kawaida kupata wasiwasi katika maisha ya kila siku. Wasiwasi huu unaweza tokana na shughuli mbalimbali za kimaisha ambazo humtaka mtu kuwa na kiwango fulani cha woga au tahadhari. Bila kujijua, ubongo wa binadamu huzalisha kiwango maalum cha wasiwasi kinachoendana na tukio husika ili kumuongezea umakini na mwishowe kumkinga asipatwe na madhara. Kama wasiwasi huu utazidi na ...

Read More »

Je unafahamu kuwa kifafa kisipotibiwa huweza kusababisha ugonjwa wa akili?

Pengine wengi tumewahi kushuhudia matukio ya watu mbalimbali wakianguka na kupoteza fahamu kunafuatiwa na mwili kutetemeka. Hali hii imekua ikishuhudiwa kutokea zaidi kwa watoto na hujulikana kama ugonjwa wa degedege. Kiuhalisia degedege si ugonjwa bali ni dalili inayoashiria matatizo katika ubongo. Matatizo haya hutokea katika mfumo wa umeme wa ubongo na huweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali lakini kwa kiasi kikubwa ...

Read More »

Thamani ya maisha ya dunia

Imepokewa Hadithi kutoka kwa Abdullah bin Masoud (Allah amridhie) kuwa siku moja Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) alilala juu ya mkeka kisha akainuka hali ya kuwa  ule mkeka umeweka alama katika ubavu wake. Maswahaba wakamwambia: “Ewe Mjumbe wa  Allah, kwa nini tusingekutengenezea tandiko?” Akasema: “Ni na nini mimi na dunia? Sikuwa mimi katika dunia isipokuwa ni kama msafiri  ambaye amepumzika kutaka kivuli chini ya mti kisha akaondoka na kuuacha,” [Tirmidhiy]. ...

Read More »

Tusiache kufunga Swaumu ya Ashura

Hakika Allah aliyetukuka ameumba majini na wanadamu kwa hekima na lengo maalum, nalo ni kumuabudu yeye, kama anavyobainisha: “Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi,” [Qur’ an, 51:56]. Na maana hasa ya ibada ni kule kuonesha udhalili na unyenyekevu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kupenda, kutukuza na kutekeleza amri zake, kadhalika kujiepusha na  aliyoyakataza. Swaumu au funga ni miongoni mwa ibada kubwa ambazo Muislamu ameusiwa kuzipenda na  kuzitekeleza. Allah Aliyetukuka amefaradhisha ...

Read More »

Swala inahitaji maandalizi-1

Swala ni nguzo ya pili katika nguzo za kiislamu, na ni ibada kongwe iliyotekelezwa na Mitume wa zama zote pamoja na wafuasi wao. Swala pia ni kigezo kikuu cha ukweli wa Uislamu wa mtu. Kuitekeleza swala ni sababu ya kukingwa na adhabu ya moto huko Akhera, kupata radhi za Allah  na kuingizwa Peponi. Vile vile kuiacha Swala ndio sababu kuu ...

Read More »

Mwaka 1440 Hijiriya, muda wa kujitathmini

Ikiwa tumeingia mwaka mpya wa 1440 Hijriya, Waislamu mbalimbali hapa nchini na duniani wamenasihiwa kujitathmini juu ya uhusiano uliopo baina yao na Muumba wao, pia, kudumisha umoja miongoni mwao kwa kuacha kufarakana kwa mujibu wa makundi. Baadhi ya Masheikh waliozungumza na gazeti imaan wamewataka Waislamu kuupokea mwaka mpya wa Hijriya kwa kuyahama maasi na kupupia mambo mema kwani hiyo ndio ...

Read More »

‘TIF Girls’ wawafariji watoto Muhimbili

Vijana wa kujitolea wa taasisi ya The Islamic Foundation upande wa wanawake (TIF Girls) wameendeleza utaratibu wao wa kujitolea kusaidia masuala anuai ya kidini na kijamii, ambapo hivi karibuni waliwatembelea watoto wenye maradhi ya vichwa vikubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa lengo la kuwafariji. Safari hiyo ni mwanzo wa azma endelevu ya kutembelea wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi tofauti ...

Read More »