Imaan Media

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy (Allah amridhie)

Wiki hii tunaanza kumzungumzia Swahaba aitwaye Salmaan al-Faarisy. Huyu ni Swahaba aliyepata umaarufu mkubwa nakupendwa sana na Waislamu kuanzia wakati wa Mtume hadi leo hii. Salmaan ambaye alitokea Fursi, (Iran ya leo), alipewa jina la ‘Assaii waraal haqiqa’ (mwenda nyuma ya haki). Jina la Salmaan kabla ya kusilimu lilikuwa ni Ruuzba bin Jashbuudhan. Ni Swahaba huyu ndie aliyeshauri Waislamu wachimbe handaki ...

Read More »

MISKI YA ROHO TENA…

Salamu alaykumu, kipazani najongea. Ndugu zangu isilamu, ujumbe nawaletea. Miski tuliyoihamu, punde tu itatujia. Roho zipate nukia, miski inatulazimu. Uturi huu muhimu, TIF yatusogezea. Mashekhe walo adhimu, toka kwetu tanzania. Hata watokao lamu, burundi uganda pia. Roho zipate nukia, miski inatulazimu. Tusiwazie ugumu, ni nafuu nawambia. Shilingi si darahimu, elfu tano kuchangia. Tiketi kila sehemu, hata kwa simu lipia. Roho ...

Read More »

Utulivu wakati wa Swala ulinifanya niingie katika Uislamu- Chacha

  Katika dini tukufu ya Uislamu kila ibada ina namna yake sahihi ya utekelezaji kutokana na mafundisho matukufu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wetu Muhammad (rehema za Allah na amani zimshukie). Uislamu ni mfumo wa maisha hivyo Mwenyezi Mungu Aliyetukuka hajaacha kitu chochote bila kukielezea hukumu na namna ya utekelezaji wake. Moja ya mafundisho ya Uislamu ni kutekeleza nguzo tano ...

Read More »

Swala inahitaji maandalizi -2

Kutokana na aya 29:45 katika Qur’an tuliyoitaja katika toleo lililopita na ambayo tutakuwa tukiirejearejea, tulijifunza kuwa,Swala ni nyenzo kubwa ya kumkinga mja na jamii kwa ujumla dhidi ya maovu na machafu. Pia, tuliona kwamba, kukingwa dhidi ya maovu, ndio haswa lengo la agizo la Muumba kwetu la kutekeleza ibada ya swala… Kazi kubwa inayomkabili kila Muislamu ni kujifunza falsafa iliyotumika ...

Read More »

WHO yakubaliana na Uislamu ubaya wa pombe

Hakuna ‘kunywa kistaarabu’ Hata glasi moja ina madhara! Ripoti mpya inayozungumzia madhara ya pombe iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Afya Duniani (WHO), inaonesha kuwa zaidi ya vifo milioni tatu duniani kote vinatokana na matumizi ya pombe. Vifo hivyo ni sawa na kifo kimoja kati ya kila 20 vinavyotokea duniani kote. Taarifa hiyo ya WHO iitwayo, ‘Ripoti ya mwaka 2018 ...

Read More »

Swala inahitaji maandalizi-3

Kabla ya kuelekea msikitini, inapendeza zaidi ukichukua udhu nyumbani. Msingi wa hili ni Qur’an. Allah Aliyetukuka anasema: “Enyi watu, chukueni mapambo yenu wakati wa kila swala, na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri) lakini msipite kiasi, hakika yeye (Mwenyezi Mungu hawapendi wapitao kiasi.” (Qur’an, 7: 32) Aya hii, licha ya kututaka tutumie neema na riziki, ikiwa ni pamoja na vyakula na ...

Read More »

Mipaka ya kuchukiana baina ya Waislamu

Kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allah [Al-walaa wal-baraa] Mpenzi msomaji, mlango wa kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allah (Al-walaa Wal-baraa) haujaishia kwa Waislamu na makafiri tu bali uko baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe. Ikiwa Muislamu ndani yake ana imani na maasia, basi atapendwa kutokana na imani yake na kuchukiwa kutokana na maasia yake. Hii iko hata katika ...

Read More »

Sharjah, TIF zafanikisha matibabu ya moyo

Wagonjwa 21, milioni 700 zaokolewa Jumuiya ya Sharjah Charity International kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imefanikiwa kuwafanyia upasuaji wa moyo jumla ya watoto 17 na watu wazima wanne katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuokoa kiasi cha Shilingi za Kitanzania zaidi ya milioni 700. Upasuaji huo ulifanyika kwa siku tatu ...

Read More »

Muhogo: Chakula Kinachotegemewa Zaidi Barani Afrika

Naam ndugu msomaji wa safu hii ya Fahamu Usiyoyajua, leo tunazungumzia mambo kadhaa kuhusu zao maarufu la muhogo. Muhogo ni moja kati ya mazao ya chakula na biashara ambalo hustahimili ukame na huweza kustawi katika udongo usio na rutuba ya kutosha. Joto linalofaa zaidi kwa ustawi wa muhogo ni kati ya nyuzi joto 25-30. Muhogo hudumaa ikiwa joto litapungua kufikia ...

Read More »

Madhara ya Uvumi kwa Amani na Usalama wa Taifa

Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe wote, na rehema na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad (saw), watu wake wa nyumbani na swahaba wake wote. Ama baada ya hayo: Ukweli wa mambo ni kuwa, uvumi na kuwaogofya watu kunazingatiwa ni kati ya silaha hatari zinazoiharibu jamii, bali mawili hayo ni kama shoka inayoiharibu dini kwa nje na ...

Read More »