Imaan Media

Tujikinge na maafa ya ulimi

Kusengenya [kuteta] Kusengenya ni moja kati ya maafa makubwa ya ulimi. Mtume [rehema za Allah na amani zimshukie] aliwauliza Maswahaba wake: “Je mnajua kusengenya ni nini?” Wakasema: “Allah na Mjumbe wake wanajua zaidi.” Akasema: “Kusengenya ni kumtaja ndugu yako kwa jambo lenye kumchukiza.” Pakasemwa: “Unaonaje kama atakuwa nalo huyo ndugu yangu hilo ninalolisema?” Akasema: “Ikiwa lipo kwake, utakuwa umemsengenya; na ...

Read More »

Tunavyoishi na majirani zetu kipimo cha wema wetu

Kumpenda jirani ni tabia njema ambayo kila mwanadamu anatakiwa aizoee na kujipamba nayo.  Uislamu ambao ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu umeifanya haki ya jirani kuwa ni haki ya kidini inayomuhusu jirani Muislamu na asiye Muislamu. Haki hizi za ujirani zinalenga kujenga moyo wa huruma na kusaidiana ili jamii ya wanadamu iishi chini ya anga la amani, utulivu, furaha na salama. ...

Read More »

Unaufahamu ugonjwa wa seli mundu?

Seli mundu au ‘sickle cell’ ni moja kati ya magonjwa makuu yanayoathiri damu moja kwa moja. Kama jina linavyojieleza, ugonjwa huu ni matokeo ya seli nyekundu za damu kubadili maumbile yake na kuwa kama mundu.Kwa takwimu zilizopo ugonjwa huu huathiri takriban watu milioni nne na nusu duniani kote ambapo asilimia 80 ya wagonjwa hupatikana katika nchi zilizo chini ya Jangwa ...

Read More »

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy (as) -2

Kutoka katika kitabu,‘Suwarun min hayati swahaba,’ Salmaan Alfarsiy, Swahaba mtukufu, anaendelea kusimulia, kuwa baada ya kuishi Ammuuriya na mwalimu wake muda aliojaaliwa, ulifika muda wa mwalimu kuiaga dunia. Salmaan Alfaarisy (Allah amridhie) alimuuliza: “Unaniusia nini baada ya wewe kuondoka?” Mwalimu wake akamjibu: “Sidhani kama kumebaki mtu yoyote juu ya mgongo huu wa ardhi aliyeshika dini sahihi hii tuliyoishika sisi. Lakini ...

Read More »

Tusiruhusu runinga na mitandao viwafunze maadili watoto wetu

Maadili kwa vijana wengi hapa nchini imekuwa ni kitu adimu sana. Miaka ya nyuma mtoto alikuwa na maadili ya hali ya juu kwa kuwa mtu yeyote alikuwa na nafasi ya kumsimamia na kumuongoza. Mwanafunzi alikuwa anamuheshimu mwalimu kama anavyowaheshimu wazee wake. Alipokemewa na mwalimu alisikiliza na kutii.Mwalimu alipomwadabisha mwanafunzi shuleni, mwanafunzi huyo alikiri na kukubali kosa. Bahati mbaya sana jambo ...

Read More »

MAMBA: Reptilia aliyeumbwa kuwinda na kuogelea

Safu hii wiki hii inakuletea habari za mamba, mnyama aina ya reptilia, mwenye umbo kubwa na anayeishi majini na nchi kavu. Mamba wanapatikana  katika Bara la Afrika, Asia, Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, na Australia Mamba wapo wa aina nyingi. Kuna alligators, cainmans, gharial. Bahati mbaya hatuna majina ya Kiswahili ya aina hizo za mamba. Mbali ya aina hizo, ...

Read More »

Wala msife ila mmekuwa Waislamu (Qur’an, 2:103)

Katika tamko hilo, amri ya kumcha Mwenyezi Mungu na kufa Muislamu inaelekezwa kwa Waumini, hivyo kuonyesha jinsi Uislamu unavyoweka umuhimu mkubwa, si tu katika maisha mazuri, bali pia kifo kizuri. Katika mazingira hayo, Waumini wanaonywa dhidi ya kubweteka, hali inayoweza kuwapeleka kwenye mwisho mbaya. Watu wengi wanajaribu kukwepa kuzungumzia kifo, licha ya ukweli kwamba kifo ni moja miongoni mwa vitu ...

Read More »

Hatua saba za kujipangia bajeti binafsi

Katika zama hizi za hali ngumu ya kiuchumi, kila mmoja anazungumzia kuwa mwangalifu zaidi na fedha. Kwa mtazamo wa Kiislamu, bila kujali hali ya uchumi, ni muhimu kuwa muangalifu na matumizi na kuweka akiba ili kuepuka israfu, kuweza kukimu familia, kuzuia madeni kadri inavyowezekana na kutenga fedha kwa ajili ya shughuli za hisani. Moja ya tabia muhimu zaidi ambazo wote ...

Read More »

Kipyenga cha Misk ya Roho 2018 Kimeshapulizwa…

Mada kuu: ‘Utukufu Wake…’ Katika muendelezo wa mfululizo wa makongamano mbalimbali yanayoandaliwa na taasisi ya The Islamic Foundation (TIF), kwa mara ya pili mtawalia tunawaletea kongamano kubwa kuwahi kutokea katika ukanda wa Afrika Mashariki litakaloendeshwa kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Misk ya Roho ni kongamano la kidaawah la Afrika Mashariki ambapo TIF, huwaalika masheikh kutoka katika nchi za Afrika ...

Read More »

Swala inahitaji maandalizi-4

Swala ya jamaa na umuhimu wake Moja ya malengo makuu ya kujengwa na kuwepo misikiti katika maeneo wanayoishi Waislamu ni kuwakusanya ili waswali pamoja, yaani swala ya jamaa. Swala ya jamaa maana yake ni watu kujumuika na kuswali pamoja nyuma ya imamu (kiongozi) mmoja wa ibada ndio maana Mtume akasisitiza kwamba, watu watatu au wawili tu wakiishi sehemu lazima waswali ...

Read More »