Imaan Media

Riziki inatoka kwa Allah peke yake!

Ufahamu kwamba ‘Rizq’ iko mkononi mwa Mwenyezi Mungu peke yake ni moja ya nguzo za ‘Aqidah’ ya Kiislamu. Ufahamu huo pia, unainua mwenendo mzima wa Muumini kuelekea kumridisha Allah ‘Azza wa Jalla’ kwa kadri inavyowezekana. Kama hiyo haitoshi, ufahamu kwamba riziki iko mkononi mwa Mwenyezi Mungu unapanua zaidi maono ya Muislamu na kumfanya afikiri tofauti kuhusu tamaa ya mali, na ...

Read More »

Sheikh: Saudi Arabia haijaharibu maeneo ya historia

Imefafanuliwa kuwa maeneo takribani yote yaliyobeba historia ya Uislamu nchini Saudi Arabia tangu enzi za Mtume Muhammad [rehema za Allah na amani zimshukie] na hata baada ya kufariki kwake, bado yanatunzwa na kulindwa tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya watu. Ufafanuzi huo umetolewa na Sheikh Haruna Jumanne Kapama katika mahojiano maalumu na gazeti imaan, akijibu tuhuma kuwa, Saudi Arabia imekuwa ...

Read More »

Sheikh Ally Jumanne achambua anga za juu

Wakati wanadamu tukichukulia dunia kama kitu kikubwa, ukweli ni kwamba sayari yetu hii tunayoishi ndani yake ni tone tu la maji katika bahari ya Mwenyezi Mungu ya uumbaji wake. Hayo yalijulikana kupitia mada iliyowasilishwa na Sheikh Ally Jumanne katika kongamano la Misk ya Roho 2018 lililofanyika katika ukumbi Diamond Jubilee jumapili iliyopita, ambapo Sheikh huyo wa Morogoro alichambua sayari za ...

Read More »

Undani wa ugonjwa wa pumu, dalili na namna ya kukabiliana nao

Pumu au ‘asthma’ ni moja kati ya magonjwa hatari sana yanayoathiri mfumo wa upumuaji ambao huathiri takriban watu million 130 duniani kote. Ingawa hakuna sababu ya moja kwa moja ya kupelekea kupata ugonjwa huu, utafiti umethibitisha ya kuwa ugonjwa huu hutokea kutokana na sababu kuu mbili, yaani vinasaba na mazingira. Nadharia ya vinasaba inatueleza kua ugonjwa huu huwapata zaidi watu ...

Read More »

Nahdi awashukuru waliohudhuria, agusia mabadiliko ya Kongamano

Mwenyekiti wa taasisi ya The Islamic Foundation [TIF], Aref Nahdi ameonesha kufurahishwa na mahudhurio makubwa ya watu katika kongamano la pili la Misk ya Roho lililofanyika Oktoba 28 mwaka huu na kubainisha kuwa anawashukuru wote waliohudhuria. Nahdi amesema mahudhurio hayo makubwa ni ishara kuwa Waislamu wanaipenda dini yao na hivyo kuwaomba wazidi kushiriki makongamano mengine ili kuusukuma mbele Uislamu. Katika ...

Read More »

Hongereni wote mliojitokeza Misk ya Roho

Oktoba 28 ya mwaka huu ilikuwa ni siku nzuri ya Waislamu hapa nchini kujumuika kwa minajili ya kupata ujumbe wa dini yao tukufu ya Uislamu. Mjumuiko huo ulifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo Waislamu walijazwa maarifa yaliyomo ndani ya dini yao tukufu ya Uislamu kutoka kwa mtoa mada mmoja hadi mwingine hadi watoa mada wote ...

Read More »

Indian cobra: Hatari ukimchokoza, lakini hana ujanja kwa tai

Utukufu ni wake Allah, Mbora wa waumbaji, Muumba wa kila kilichopo ulimwengu kwa sifa tofauti. Juma hili tukauone ukubwa wa Allah Aliyetukuka kwa kumsoma nyoka aitwaye Indian Cobra, miongoni mwa aina ya nyoka hatari katika kundi la epidae. Wengi wanaaminu kuna nyoka mmoja tu aitwaye cobra, lakini ukweli ni kwamba kuna aina takriban 270 za viumbe za cobra. Hata hivyo, ...

Read More »

Tushirikiane na walimu kuwaelimisha watoto

Ni ndoto ya kila mzazi kuona mtoto wake anafanya vizuri katika elimu, iwe ya dini au mazingira. Wazazi wengi hujinyima na kutumia rasilimali zao kufahakikisha watoto wao wanapata elimu bora. Hili ni jambo zuri na linalofaa kupongezwa. Hongereni sana wazazi. Endeleeni na moyo huohuo. Lakini, wapo wazazi ambao wanaona suala la kumuelimisha mtoto ni kazi ya mwalimu. Mtoto anapofanya vibaya ...

Read More »

MAISHA YA MASWAHABA: Salmaan al-Faarisy, Maisha yake baada ya kusilimu

Kutokana na maelezo yaliyotangulia tunajifunza kwamba Salmaan alisilimu mwaka wa kwanza Hijriya mara tu baada ya Mtume [rehema za Allah na amani zimshukie] kuwasili Madina. Kuanzia hapo aliishi na Mtume na inasemekana alikuwa muachwa huru wake, kwa maana Mtume alimlipia gharama za kumkomboa. Na pia Salmaan anatajwa kuwa ni katika watu aliyowapa hadhi yakuwa mtu wa nyumbani mwake [Ahlu bayti]. ...

Read More »

Fahamu undani wa ugonjwa wa TB, dalili na namna ya kujikinga

TB au kifua kikuu ni moja kati ya magonjwa hatari sana yanayoathiri mfumo wa upumuaji. Kwa lugha ya kitaalamu ugonjwa huu hujulikana kama ‘tuberculosis’ na husababishwa na bakteria hatari wajulikanao kama ‘Mycobacterium tuberculosis’. Ugonjwa huu bado umekua tishio kubwa katika katika nchi za Afrika kwani mpaka sasa, takriban asilimia 95 ya wagonjwa wote wa TB hupatikana katika bara hili. Namna ...

Read More »