Imaan Media

Ishara za uwepo wa Mwenyezi Mungu Muumba kupitia miujiza ya Qur’an

Baada ya Allah Aliyetukuka kumuumba mwanadamu na kumleta katika uhai huu, alimpa majukumu mengi ili ayatekeleze. Utekelezaji wa majukumu hayo maana yake ni kumuabudu Yeye, Allah. Miongoni mwa majukumu hayo, la awali kabisa ni kwanza, kumtambua Yeye, Mwenyezi Mungu, kwa dhati. Kwa vile Allah hana sifa ya kuonekana katika maisha ya dunia, pia hashikiki, hagusiki na wala hadirikiwi kupitia milango ...

Read More »

Miongoni mwa Alama za Kiyama

Twariq [Allah amrehemu] amehadithia kuwa, walikuwa wamekaa kwa Abdullah bin Mas’oud [Allah amridhie]. Mara muadhini wake akaja, akasema: “Qad qaamati Swalaa” akiwatanabahisha kuwa ni wakati wa Swala. Ibnu Mas’oud(ra) alisimama, nao wakasimama pamoja naye, wakaingia msikitini. Akawaona watu wamerukuu; akatoa takbira halafu akarukuu. Nao wakaenda na kufanya alivyofanya. Wakati wanaswali, akapita mtu mmoja kwa haraka, akasema: “Amani ikushukie Abuu AbdirRahman,” ...

Read More »

Swala, mnyama aliyetawaliwa na wasiwasi

Ndugu yangu msomaji, dunia ya Muumba wetu Allah, mbora wa uumbaji, ina mapambo mengi. Ukiachilia mbali milima, bahari, mito, maziwa, majangwa; pia kuna wanyama wa aina nyingi. Wanyama hawa ni hisani kutoka kwa Muumba wa mbingu na ardhi kwa ajili yetu sisi wanadamu. Ninapozungumzia tabia za wanyama na viumbe wengine; nauona ukubwa na uwezo wa Muumbaji katika fikra zangu. Katika ...

Read More »

Udhalilishaji wa watoto: Wahusika wakubwa ni ndugu wa karibu

Vitendo vya udhalilishaji wa watoto vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku. Serikali, mashirika ya kiraia na wadau mbalimbali wamekuwa wakitafuta njia mbalimbali za kukabiliana na hali hii. Tunaposema udhalilishaji tunajumuisha mambo yote mabaya yenye kumdhulumu mtoto utu wake na mara nyingi hufanywa kwa siri. Baadhi ya matendo haya huambatana na unyanyasaji wa kingono kama vile kubaka na kulawiti nk. Kwa jumla, ...

Read More »

Fahamu dalili za upungufu wa vitamini katika mwili

Vitamini ni moja kati ya viini lishe muhimu sana katika mwili wa binaadamu. Umuhimu huu unatokana na shughuli mbalimbali ambazo ufanisi wa kufanyika kwake hutegemea vitamini. Kabla ya kujionea dalili mbalimbali ambazo hutokea katika mwili, ni vyema tukatambua kazi mbalimbali za viini lishe hivi. Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na kuboresha afya ya meno, mifupa, ngozi, kutengeneza damu, kugandisha ...

Read More »

Mufti akemea ushoga

Wakati mijadala ya sakata la ushoga likiendelea nchini na duniani, Mufti  Sheikh Abubakar Zubeir ametoa neno lake na kusema, vitendo hivyo vichafu havikubaliki ndani ya Uislamu na jamii kwa ujumla. Mufti Zubeir aliwaambia waandishi wa habari kuwa, vitendo vya kishoga ni kiashiria kibaya cha mmomonyoko wa maadili katika jamii: “Uislamu haukubali ushoga, Uislamu unakataza juu ya masuala haya, kwa sababu ...

Read More »

Faida za vikao vya kumtaja Allah- 1

Mwanadamu ni mwanajamii na kwa tabia yake ya kimaumbile kamwe hawezi kuishi maisha ya kujitenga; na akifanya hivyo atapata matatizo. Uthibitisho wa hili ni hali ya mabedui (Waarabu wa mashambani) katika zama za Mtume (rehema za Allah na amani zimshukie) ambao walikuwa wakiishi maisha ya kujitenga na watu, jambo ambalo lilimkera Mtume na Maswahaba zake (Allah awaridhie). Pamoja na kupenda ...

Read More »

Tanzania kugeuka taifa la wacheza kamari?

Gazeti la Imaan mara nyingi limekuwa likiandika habari za madhara ya kamari, kiasi kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakidhani chombo hiki kinatia chumvi tu na kwamba madhara si makubwa kihivyo!! Kama ulikuwa unafikiria hivyo fikiria upya; kwani, sasa hivi hadi maprofesa katika vyuo vikuu mbalimbali wabobezi katika utafiti na tafakuri za kina wanaona madhara ya kamari kiasi cha kuibua suala ...

Read More »

Tuziunge mkono taasisi za dini kuwekeza sekta ya elimu

Miongoni mwa habari zilizowahi kuandikwa katika toleo la gazeti Imaan ni inayohusu taasisi ya Direct Aid yenye makao yake makuu nchini Kuwait ikisema kuwa itazidi kuwekeza kwenye sekta ya elimu hapa nchini na kwingineko duniani. Zaidi, taasisi hiyo imesema kuwa, huwa inatumia asilimia 80 ya bajeti yake katika sekta hiyo, kama alivyobainisha Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dkt. Abdallah Al Subayt. ...

Read More »

Zifahamu faida mbalimbali za mbegu za maboga

Kwa miaka ya zamani mbegu za maboga zilionekana kitu ambacho hakina faida hivyo wengi mwa wanajamii walikua wakizitupa. Kwa haraka, tunaweza kusema mbegu hizi zilikuwa zikitupwa pengine kutokana na kutojua faida zake, hususan uwepo wa virutubisho mbalimbali ambayo vina faida nyingi sana katika mwili wa binadamu. Katika makala hii, ntakujulisha faida hizi ambazo miili yetu hupata ikiwa tutazitumia mbegu za ...

Read More »