Fahamu Usiyoyajua

Bimbirisa Kimba [Beetle] Mdudu maarufu kwa kuviringisha kinyesi

Naam Ndugu yangu mfuatiliaji na msomaji wa safu hii ya ‘Fahamu usiyoyajua’, juma hili nataka nikufahamishe mambo mengi yamuhusuyo mdudu mwenye majina mengi. Baadhi ya Waswahili humuita, bimbirisa kimba, wadigo humuita ‘chidundu’. Pia wapo muitao ‘tuta.’ Waingereza wao humuita ‘beetle.’ Hawa ni wadudu walio maarufu sana. Wana miguu sita; kulia mitatu, kushoto mitatu, ingawa Allah Aliyetukuka amewatofautisha na wadudu wengine ...

Read More »

DEAD SEA: Bahari isiyo na viumbe hai, kila kitu kinaelea!

Kila kilichomo mbinguni ni ushahidi wa uwepo wa Mwenyezi  Mungu, Muweza na Mmoja  aliye Mpweke. Yeye, Mwenyezi  Mungu ni Mwenye nguvu na uwezo  usioshindwa. Yeye ni Mwenye hekima kwa utaratibu wake alioupanga  ambao hatokei kuupinga mtu ila aliye jahili au mwenye kiburi. Mwenyezi Mungu ameumba mbingu bila ya nguzo mnazoziona na ameweka katika ardhi milima ili ardhi isiwayumbishe. Pia, Mwenyezi Mungu ametawanya humo kila ...

Read More »

MENDE: wadudu wastahamilivu, waishio kwenye hali zote za hewa

Naam ndugu yangu msomaji wa safu hii ya ‘Fahamu Usiyoyajua’ juma hili nataka tukajifunze kuhusu mdudu aina ya mende. Kwa wale wasiomfahamu, mende hawa ni wadudu wenye miguu sita, upande wa kushoto miguu mitatu, na upande wa kulia miguu mitatu. Mende wana taya za kutafunia, miili iliyokuwa bapa, na kichwa kidogo. Wengi wao wana rangi nyekundu, kahawia mpaka nyeusi. Macho ...

Read More »

Swala, mnyama aliyetawaliwa na wasiwasi

Ndugu yangu msomaji, dunia ya Muumba wetu Allah, mbora wa uumbaji, ina mapambo mengi. Ukiachilia mbali milima, bahari, mito, maziwa, majangwa; pia kuna wanyama wa aina nyingi. Wanyama hawa ni hisani kutoka kwa Muumba wa mbingu na ardhi kwa ajili yetu sisi wanadamu. Ninapozungumzia tabia za wanyama na viumbe wengine; nauona ukubwa na uwezo wa Muumbaji katika fikra zangu. Katika ...

Read More »

Indian cobra: Hatari ukimchokoza, lakini hana ujanja kwa tai

Utukufu ni wake Allah, Mbora wa waumbaji, Muumba wa kila kilichopo ulimwengu kwa sifa tofauti. Juma hili tukauone ukubwa wa Allah Aliyetukuka kwa kumsoma nyoka aitwaye Indian Cobra, miongoni mwa aina ya nyoka hatari katika kundi la epidae. Wengi wanaaminu kuna nyoka mmoja tu aitwaye cobra, lakini ukweli ni kwamba kuna aina takriban 270 za viumbe za cobra. Hata hivyo, ...

Read More »

MAMBA: Reptilia aliyeumbwa kuwinda na kuogelea

Safu hii wiki hii inakuletea habari za mamba, mnyama aina ya reptilia, mwenye umbo kubwa na anayeishi majini na nchi kavu. Mamba wanapatikana  katika Bara la Afrika, Asia, Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, na Australia Mamba wapo wa aina nyingi. Kuna alligators, cainmans, gharial. Bahati mbaya hatuna majina ya Kiswahili ya aina hizo za mamba. Mbali ya aina hizo, ...

Read More »

Muhogo: Chakula Kinachotegemewa Zaidi Barani Afrika

Naam ndugu msomaji wa safu hii ya Fahamu Usiyoyajua, leo tunazungumzia mambo kadhaa kuhusu zao maarufu la muhogo. Muhogo ni moja kati ya mazao ya chakula na biashara ambalo hustahimili ukame na huweza kustawi katika udongo usio na rutuba ya kutosha. Joto linalofaa zaidi kwa ustawi wa muhogo ni kati ya nyuzi joto 25-30. Muhogo hudumaa ikiwa joto litapungua kufikia ...

Read More »

Mdudu Hatari Lakini Haumi

Msomaji wa Fahamu Usiyoyajua, juma hili ninakujuza tabia za mdudu aitwaye, ‘Nairobi Fly.’ Huyu ni jamii ya wadudu wanaopenda kuviringisha kinyesi, kwa Kiswahili ‘Tuta wale,’ kwa Kiingereza ‘Beettle’ lakini wadigo wanamuita Chidundu. Nairobi fly ana miguu sita; kulia mitatu na kushoto mitatu, lakini haruki. Pia, ana antenna mbili. Wadudu hawa, kwa mbele wana rangi nyekundu na nyeusi, na ukubwa wao ...

Read More »

Sungura mnyama anayekula kinyesi chake | Fahamu Usiyoyajua

Naam, ndugu yangu msomaji, sungura ni kiumbe anayepatikana karibu maeneo yote duniani isipokuwa sehemu za ncha ya kaskazini. Inaelezwa kuwa nusu ya sungura wote duniani wapo katika bara la Amerika ya Kaskazini. Wanyama hawa wanajulikana kwa masikio yao marefu yaliyoelekea juu, miguu minne; miwili mbele na miwili nyuma. Tofauti na wanyama wengine, miguu ya nyuma ya sungura ina nguvu zaidi kuliko ...

Read More »

Ndege Mzuri Mwenye Madaha: Tausi

Naam ndugu msomaji wa safu hii ya ‘Fahamu Usiyoyajua,’ juma hili ninakuletea dondoo za ajabu kuhusina na ndege anayevutia machoni na mwenye madaha, tausi. Tausi ni ndege maarufu aliyewashangaza na anayeendelea kuwashangaza watafiti kwa namna Mwenyezi Mungu Aliyetukuka alivyomuumba. Tausi ana mdomo mrefu kiasi, manyoya mengi yaliyopambwa kwa rangi mbalimbali nzuri zenye kung’aa ajabu. Miongoni mwa rangi hizo ni kijani ...

Read More »