Afya Yako

Zifahamu faida mbalimbali za mbegu za maboga

Kwa miaka ya zamani mbegu za maboga zilionekana kitu ambacho hakina faida hivyo wengi mwa wanajamii walikua wakizitupa. Kwa haraka, tunaweza kusema mbegu hizi zilikuwa zikitupwa pengine kutokana na kutojua faida zake, hususan uwepo wa virutubisho mbalimbali ambayo vina faida nyingi sana katika mwili wa binadamu. Katika makala hii, ntakujulisha faida hizi ambazo miili yetu hupata ikiwa tutazitumia mbegu za ...

Read More »

Undani wa ugonjwa wa pumu, dalili na namna ya kukabiliana nao

Pumu au ‘asthma’ ni moja kati ya magonjwa hatari sana yanayoathiri mfumo wa upumuaji ambao huathiri takriban watu million 130 duniani kote. Ingawa hakuna sababu ya moja kwa moja ya kupelekea kupata ugonjwa huu, utafiti umethibitisha ya kuwa ugonjwa huu hutokea kutokana na sababu kuu mbili, yaani vinasaba na mazingira. Nadharia ya vinasaba inatueleza kua ugonjwa huu huwapata zaidi watu ...

Read More »

Fahamu undani wa ugonjwa wa TB, dalili na namna ya kujikinga

TB au kifua kikuu ni moja kati ya magonjwa hatari sana yanayoathiri mfumo wa upumuaji. Kwa lugha ya kitaalamu ugonjwa huu hujulikana kama ‘tuberculosis’ na husababishwa na bakteria hatari wajulikanao kama ‘Mycobacterium tuberculosis’. Ugonjwa huu bado umekua tishio kubwa katika katika nchi za Afrika kwani mpaka sasa, takriban asilimia 95 ya wagonjwa wote wa TB hupatikana katika bara hili. Namna ...

Read More »

Unaufahamu ugonjwa wa seli mundu?

Seli mundu au ‘sickle cell’ ni moja kati ya magonjwa makuu yanayoathiri damu moja kwa moja. Kama jina linavyojieleza, ugonjwa huu ni matokeo ya seli nyekundu za damu kubadili maumbile yake na kuwa kama mundu.Kwa takwimu zilizopo ugonjwa huu huathiri takriban watu milioni nne na nusu duniani kote ambapo asilimia 80 ya wagonjwa hupatikana katika nchi zilizo chini ya Jangwa ...

Read More »

Jikinge na Bawasili Kwa Kubadili Mfumo wa Maisha

Bawasili ni moja ya magonjwa maarufu zaidi yanayoathiri mfumo wa chakula hususan njia ya haja kubwa. Wataalamu huita ugonjwa huu ‘hemorrhoids,’ jina ambalo limetokana na kuvimba na kuchomoza kwa mishipa ya damu inayopatikana katika puru (rectum) na mlango wa haja kubwa. Mishipa hii hujulikana kama ‘hemorrhoidal veins’ na kazi yake kubwa ni kusafirisha damu kwenda kwenye moyo na inaweza kuchomoza ...

Read More »

Je, ni woga wa kawaida au ugonjwa wa wasiwasi? | Afya yako

  Ni jambo la kawaida kupata wasiwasi katika maisha ya kila siku. Wasiwasi huu unaweza tokana na shughuli mbalimbali za kimaisha ambazo humtaka mtu kuwa na kiwango fulani cha woga au tahadhari. Bila kujijua, ubongo wa binadamu huzalisha kiwango maalum cha wasiwasi kinachoendana na tukio husika ili kumuongezea umakini na mwishowe kumkinga asipatwe na madhara. Kama wasiwasi huu utazidi na ...

Read More »

Je unafahamu kuwa kifafa kisipotibiwa huweza kusababisha ugonjwa wa akili?

Pengine wengi tumewahi kushuhudia matukio ya watu mbalimbali wakianguka na kupoteza fahamu kunafuatiwa na mwili kutetemeka. Hali hii imekua ikishuhudiwa kutokea zaidi kwa watoto na hujulikana kama ugonjwa wa degedege. Kiuhalisia degedege si ugonjwa bali ni dalili inayoashiria matatizo katika ubongo. Matatizo haya hutokea katika mfumo wa umeme wa ubongo na huweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali lakini kwa kiasi kikubwa ...

Read More »

‘TIF Girls’ wawafariji watoto Muhimbili

Vijana wa kujitolea wa taasisi ya The Islamic Foundation upande wa wanawake (TIF Girls) wameendeleza utaratibu wao wa kujitolea kusaidia masuala anuai ya kidini na kijamii, ambapo hivi karibuni waliwatembelea watoto wenye maradhi ya vichwa vikubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa lengo la kuwafariji. Safari hiyo ni mwanzo wa azma endelevu ya kutembelea wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi tofauti ...

Read More »

Je, Unayajua Madhara Ya Sigara Katika Mwili?

Sigara ni moja ya vileo vinavyotumiwa na idadi kubwa ya watu. Wengi huamini kuwa pengine sigara haina madhara yoyote, kadhalika wapo wanaoamini kuwa yapo madhara madogo ambayo mtu anaweza kuyapata ikiwa atavuta sigara kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, imethibitika kuwa sigara huathiri takriban mifumo yote mikuu ya mwili, lakini kwa kiasi kikubwa mfumo wa upumuaji ndio huathirika ...

Read More »

Jinsi ya kugundua saratani ya matiti kwa kutumia macho na mikono yako

Saratani ya matiti imekuwa ugonjwa tishio kwa wanawake. Wataalamu wanaitaja kama saratani hatari zaidi ikiongoza kusababisha vifo kwa wanawake kuliko saratani nyingine zote. Wasichokijua baadhi ya watu ni kuwa, kwa kiasi kidogo saratani hii pia inaweza kuwapata wanaume. Namna inavyotokea Ndugu msomaji, elewa ya kua mwili wote wa binadamu umejengwa na seli. Seli hizi huishi kwa muda kisha hufa na kuzaliwa ...

Read More »