Gazeti Imaan

Zifahamu faida mbalimbali za mbegu za maboga

Kwa miaka ya zamani mbegu za maboga zilionekana kitu ambacho hakina faida hivyo wengi mwa wanajamii walikua wakizitupa. Kwa haraka, tunaweza kusema mbegu hizi zilikuwa zikitupwa pengine kutokana na kutojua faida zake, hususan uwepo wa virutubisho mbalimbali ambayo vina faida nyingi sana katika mwili wa binadamu. Katika makala hii, ntakujulisha faida hizi ambazo miili yetu hupata ikiwa tutazitumia mbegu za ...

Read More »

Undani wa ugonjwa wa pumu, dalili na namna ya kukabiliana nao

Pumu au ‘asthma’ ni moja kati ya magonjwa hatari sana yanayoathiri mfumo wa upumuaji ambao huathiri takriban watu million 130 duniani kote. Ingawa hakuna sababu ya moja kwa moja ya kupelekea kupata ugonjwa huu, utafiti umethibitisha ya kuwa ugonjwa huu hutokea kutokana na sababu kuu mbili, yaani vinasaba na mazingira. Nadharia ya vinasaba inatueleza kua ugonjwa huu huwapata zaidi watu ...

Read More »

Indian cobra: Hatari ukimchokoza, lakini hana ujanja kwa tai

Utukufu ni wake Allah, Mbora wa waumbaji, Muumba wa kila kilichopo ulimwengu kwa sifa tofauti. Juma hili tukauone ukubwa wa Allah Aliyetukuka kwa kumsoma nyoka aitwaye Indian Cobra, miongoni mwa aina ya nyoka hatari katika kundi la epidae. Wengi wanaaminu kuna nyoka mmoja tu aitwaye cobra, lakini ukweli ni kwamba kuna aina takriban 270 za viumbe za cobra. Hata hivyo, ...

Read More »

Fahamu undani wa ugonjwa wa TB, dalili na namna ya kujikinga

TB au kifua kikuu ni moja kati ya magonjwa hatari sana yanayoathiri mfumo wa upumuaji. Kwa lugha ya kitaalamu ugonjwa huu hujulikana kama ‘tuberculosis’ na husababishwa na bakteria hatari wajulikanao kama ‘Mycobacterium tuberculosis’. Ugonjwa huu bado umekua tishio kubwa katika katika nchi za Afrika kwani mpaka sasa, takriban asilimia 95 ya wagonjwa wote wa TB hupatikana katika bara hili. Namna ...

Read More »

Unaufahamu ugonjwa wa seli mundu?

Seli mundu au ‘sickle cell’ ni moja kati ya magonjwa makuu yanayoathiri damu moja kwa moja. Kama jina linavyojieleza, ugonjwa huu ni matokeo ya seli nyekundu za damu kubadili maumbile yake na kuwa kama mundu.Kwa takwimu zilizopo ugonjwa huu huathiri takriban watu milioni nne na nusu duniani kote ambapo asilimia 80 ya wagonjwa hupatikana katika nchi zilizo chini ya Jangwa ...

Read More »

MAMBA: Reptilia aliyeumbwa kuwinda na kuogelea

Safu hii wiki hii inakuletea habari za mamba, mnyama aina ya reptilia, mwenye umbo kubwa na anayeishi majini na nchi kavu. Mamba wanapatikana  katika Bara la Afrika, Asia, Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, na Australia Mamba wapo wa aina nyingi. Kuna alligators, cainmans, gharial. Bahati mbaya hatuna majina ya Kiswahili ya aina hizo za mamba. Mbali ya aina hizo, ...

Read More »

Swala inahitaji maandalizi-3

Kabla ya kuelekea msikitini, inapendeza zaidi ukichukua udhu nyumbani. Msingi wa hili ni Qur’an. Allah Aliyetukuka anasema: “Enyi watu, chukueni mapambo yenu wakati wa kila swala, na kuleni (vizuri) na kunyweni (vizuri) lakini msipite kiasi, hakika yeye (Mwenyezi Mungu hawapendi wapitao kiasi.” (Qur’an, 7: 32) Aya hii, licha ya kututaka tutumie neema na riziki, ikiwa ni pamoja na vyakula na ...

Read More »

Muhogo: Chakula Kinachotegemewa Zaidi Barani Afrika

Naam ndugu msomaji wa safu hii ya Fahamu Usiyoyajua, leo tunazungumzia mambo kadhaa kuhusu zao maarufu la muhogo. Muhogo ni moja kati ya mazao ya chakula na biashara ambalo hustahimili ukame na huweza kustawi katika udongo usio na rutuba ya kutosha. Joto linalofaa zaidi kwa ustawi wa muhogo ni kati ya nyuzi joto 25-30. Muhogo hudumaa ikiwa joto litapungua kufikia ...

Read More »

Madhara ya Uvumi kwa Amani na Usalama wa Taifa

Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe wote, na rehema na amani zimfikie Mtume wetu Muhammad (saw), watu wake wa nyumbani na swahaba wake wote. Ama baada ya hayo: Ukweli wa mambo ni kuwa, uvumi na kuwaogofya watu kunazingatiwa ni kati ya silaha hatari zinazoiharibu jamii, bali mawili hayo ni kama shoka inayoiharibu dini kwa nje na ...

Read More »

Jikinge na Bawasili Kwa Kubadili Mfumo wa Maisha

Bawasili ni moja ya magonjwa maarufu zaidi yanayoathiri mfumo wa chakula hususan njia ya haja kubwa. Wataalamu huita ugonjwa huu ‘hemorrhoids,’ jina ambalo limetokana na kuvimba na kuchomoza kwa mishipa ya damu inayopatikana katika puru (rectum) na mlango wa haja kubwa. Mishipa hii hujulikana kama ‘hemorrhoidal veins’ na kazi yake kubwa ni kusafirisha damu kwenda kwenye moyo na inaweza kuchomoza ...

Read More »