Imaan Media

Umaskini bado kikwazo cha elimu kwa jamii za Waislamu

Wakati tukielekea mwishoni mwa mwaka ambapo shule za msingi na sekondari hufungwa, tayari kwa maandalizi ya mwaka mpya wa msomo utakaoanza Januari, uchunguzi wa gazeti la Imaan  unaonesha kuwa, umaskini ufukara bado ni kikwazo kikubwa kwa jamii za Kiislamu katika kuitafuta elimu, hususan ya mazingira. Athari ya ufukara na umaskini inaonekana wazi kwa familia zenye watoto ambao wamemaliza ngazi moja ya elimu ...

Read More »

Kunguni: Bila damu hana maisha

Uhai hauwezi kuwa ulitokea tu,  bali yupo aliyeuleta; na huyo aliyeuleta, Mwenyezi Mungu, Muumba ameuleta uhai kwa mpango, hekima na makusudi maalumu. Katika safu yetu hii inayolenga kuimarisha msimamo wako juu ya  uwepo wa Allah Aliyetukuka kupitia maajabu ya uumbaji wake, leo tunamuangazia mdudu kunguni. Kunguni ni katika wadudu wenye maajabu sana. Mdudu huyu haruki, bali hutambaa. Ni mdudu mdogo aliyejaaliwa miguu ...

Read More »

Bimbirisa Kimba [Beetle] Mdudu maarufu kwa kuviringisha kinyesi

Naam Ndugu yangu mfuatiliaji na msomaji wa safu hii ya ‘Fahamu usiyoyajua’, juma hili nataka nikufahamishe mambo mengi yamuhusuyo mdudu mwenye majina mengi. Baadhi ya Waswahili humuita, bimbirisa kimba, wadigo humuita ‘chidundu’. Pia wapo muitao ‘tuta.’ Waingereza wao humuita ‘beetle.’ Hawa ni wadudu walio maarufu sana. Wana miguu sita; kulia mitatu, kushoto mitatu, ingawa Allah Aliyetukuka amewatofautisha na wadudu wengine ...

Read More »

Waislamu watakiwa kuwekeza sekta ya elimu

Wadau wa elimu hapa nchini wametakiwa kuwekeza kwenye sekta ya elimu ili kuwawezesha vijana kupata elimu bora inayoendana na matakwa halisi ya ulimwengu wa leo. Wito huo umetolewa na Muhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Pazi Mwinyimvua wakati wa mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne na elimu ya awali katika shule za Yemen DYCCC, ...

Read More »

Undani wa saratani ya shingo ya kizazi na namna ya kupambana nayo

Pengine huenda neno hili likawa linatisha zaidi kwa wagonjwa ‘una saratani’. Kwa ujumla saratani inajumuisha kundi kubwa la magonjwa ambayo husababisha ukuaji wa seli usio wa kawaida. Seli hizi huweza kukua na kuvuka mipaka yake na muda mwengine seli hizi huweza kusambaa na kuenea katika viungo vyengine. Kwa kitaalamu saratani hujulikana kama ‘cancer’, ‘malignant tumour’ au ‘neoplasm’.Kwa takwimu za jumla ...

Read More »

DEAD SEA: Bahari isiyo na viumbe hai, kila kitu kinaelea!

Kila kilichomo mbinguni ni ushahidi wa uwepo wa Mwenyezi  Mungu, Muweza na Mmoja  aliye Mpweke. Yeye, Mwenyezi  Mungu ni Mwenye nguvu na uwezo  usioshindwa. Yeye ni Mwenye hekima kwa utaratibu wake alioupanga  ambao hatokei kuupinga mtu ila aliye jahili au mwenye kiburi. Mwenyezi Mungu ameumba mbingu bila ya nguzo mnazoziona na ameweka katika ardhi milima ili ardhi isiwayumbishe. Pia, Mwenyezi Mungu ametawanya humo kila ...

Read More »

Muonekano wa Uislamu kwa watu wa Kitabu na namna ya kuamiliana nao

Hakika Uislamu ni dini aliyokuja nayo Mtume Mtukufu Muhammad (rehema za Allah na amani zimshukie) toka kwa Mwenyezi Mungu, Mola mlezi wa ulimwengu. Amesema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: “Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu.” (Quran, 3: 19). Na hii ni baada ya Mola wetu kuiridhia dini hii kwetu na pia kutimiza neema zake kwetu. Amesema Mwenyezi Mungu ...

Read More »

Tetekuwanga: Ukiugua mara moja umepata kinga ya kudumu

Wengi tumezoea kuona ugonjwa huu ukiwaathiri watoto kwa kiasi kikubwa. Lakini ukweli ni kuwa, mbali watoto, ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yeyote ikiwa atagusana na virusi aina ya ‘Varicella zoster’. Ugonjwa wa tetekuwanga au kwa kitaalamu ‘chickenpox’ ni moja kati ya magonjwa ya muda mfupi yanayosambaa kwa kasi sana. Ugonjwa huu huitwa ugonjwa wa muda mfupi kwa sababu husababisha dalili ...

Read More »

MENDE: wadudu wastahamilivu, waishio kwenye hali zote za hewa

Naam ndugu yangu msomaji wa safu hii ya ‘Fahamu Usiyoyajua’ juma hili nataka tukajifunze kuhusu mdudu aina ya mende. Kwa wale wasiomfahamu, mende hawa ni wadudu wenye miguu sita, upande wa kushoto miguu mitatu, na upande wa kulia miguu mitatu. Mende wana taya za kutafunia, miili iliyokuwa bapa, na kichwa kidogo. Wengi wao wana rangi nyekundu, kahawia mpaka nyeusi. Macho ...

Read More »

Kuwa makini na utapeli: upotoshaji katika ‘tiba ya Kisunna’

Kitambo sasa tangu iingie tiba dhidi ya majini na mashetani ijulikanayo kama ‘tiba ya kisunna’ na wengine wakiita ‘tiba mbadala.’ Lakini, je tiba hii kweli inakidhi viwango vya kuitwa tiba ya Kisunna? Ni jambo la kushukuriwa kwamba wanaojishughulisha na tiba hii ya Kisunna wamerejesha imani ya watu kuhusu Qur’an na Sunna kwani kuna kipindi, waliokumbwa na mashetani walikimbilia katika mahubiri ...

Read More »